KONA YA BIASHARA: Ongezeka Wewe Kwanza.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kwenye biashara nyingi unaweza kukutana na watu wanalalamika biashara zao hazikui, hakuna kinachoongezeka hali ni ile kwa muda mrefu. Ukija kuchunguza Zaidi unakutana na shida nyingine kwamba mmiliki wa biashara mwenyewe hajakua.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba biashara haiwezi kukua inakuzidi wewe. Kile kiwango cha ukuaji wa biashara yako ni kiwango chako cha ukuaji. Ule uwezo wako wa umiliki wa fedha ndio hapo utaishia pia kwenye unachomiliki kwenye biashara yako.

Kabla hujalaumu hali ngumu, hakuna wateja, jitazame wewe binafsi ni kwa kiwango gani umejifunza ili kuendana na ukuaji wa biashara yako. Biashara tunaweza kuipa mfano wa gari Kadiri linavyoongezeka kasi ndio uwezekano wa dereva kuliangusha unakuwa mkubwa. Kama dereva atashindwa kuendana na kasi ya gari ni bora akapunguza mwendo au akubali kukutana na ajali mbele.

Hivyo pia kwenye biashara kasi ya ukuaji wa biashara ni kasi ya ukuaji wako binafsi wewe mwenye maono ya biashara hiyo. Kama utashindwa kuendana na kasi utapata wateja wengi mwisho wa siku utashindwa kuwahudumia. Utapata faida kubwa mwisho wa siku utalewa mafanikio na kupoteza kila ulichonacho.

Tenga muda binafsi wa kujifunza na kusoma vitabu. Tafuta muda wa kufuatilia biashara kubwa kuliko hiyo yako wanaendeshaje biashara zao. Hakuna namna nyingine labda tu uwe umeamua kubakia hapo ulipo.

Ili uweze kumiliki mtaji mkubwa lazima kiwango chako cha umiliki wa fedha ndani yako kiongezeke la sivyo utashindwa kuendesha biashara yako.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading