Nimekuwa nakutana na watu wengi wanatamani sana kuingia kwenye biashara ukija kuwauliza ni kitu gani hasa kinawasukumu waingie watakwambia kuna matatizo Fulani wanataka wayatatue. Sasa watu wa aina hii wanakuwaga ni majanga sana kwasababu ataanza baada ya muda Fulani watu wamemzoea hivi yeye anakuwa amemaliza shida zake anaacha biashara.

Vilevile anaweza kukutana na changamoto kidogo akakata tamaa haraka sana kwasababu yeye alitaka apate faida za haraka kisha aachane na biashara hiyo. Sio vibaya lakini unakuwa unatengeneza shida nyingine. Kuna watu wataanza kukuamini na kuacha kwenda sehemu nyingine ghafla unaacha biashara ujue hawa hawataweza tena kuja kukuamini ukianzisha kitu kingine.

Kama unaanza biashara kwa matatizo yako ya msimu ujue utakuja kuwaumiza watu bure. Kama unaanza biashara ili upate fedha au kwasababu ulikuwa huna kitu cha kufanya bado na wewe ni tatizo. Utakuja kuwasumbua watu huku mtaani bure.

Sababu za Kudumu;

Sababu nyingine ni sababu za kudumu hapa unakuta mtu ana msukumo wa kufanya biashara ndani yake sio tu kwasababu ana shida ya pesa bali ni kwa kupenda. Mtu huyu atapenda kuona ni vitu gani havipo sehemu aliyopo na atajitahidi aanze kuuza. Ataangalia ni tatizo gani lipo sehemu aliyopo alitatue.

Mtu huyu ukitokea ukaiga biashara yake wala hana ugomvi na wewe anaweza kukuachia akaanzisha nyingine nab ado akawaelekeza wateja wako waje kwako. Mtu huyu ni mojawapo ya watu ambao wanaweza kuvumilia changamoto za aina mbalimbali wanazokutana nazo kwenye biashara. Mtu huyu anaweza kudumu kwenye biashara kwa muda mrefu sana.

Hata kama anatafuta pesa basi huyu anakuwa anatafuta uhuru wa kipesa sio pesa za kutatua matatizo Fulani basi. Maana yake anataka akuze biashara isimame na ijiendeshe yenyewe hata kama hayupo yeye. Mtu huyu kufanikiwa kwake inawezekana.

Ukiingia kwenye biashara kwa matatizo yako ya muda mfupi basi hakikisha hata biashara yako sio ya kudumu.

Kama ni kumshauri mtu anaekuja anataka kufanya biashara napenda kujua kwanza ni kitu gani kinamsukuma aje kwenye biashara?

Ukiwa na sababu nzuri ndipo utaweza kufanikiwa. Ukiwa na sababu mbaya ni rahisi sana kuishia njiani.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading