KONA YA BIASHARA: Ukipoteza Hii Inakuja Nyingine.

jacobmushi
2 Min Read

Kuna nyakati kwenye Maisha unaweza kujiona umepoteza vitu vikubwa sana na ukaanza kuona kama Maisha hayana maana tena. Unachopaswa kutambua ni kwamba kila kinapoondoka kitu basi kuna kitu kingine kipya kinatokea.

Mti unapokauka unakuwa umetoa nafasi kwa miti mingine mingi midogo kukua vizuri. Chochote kinachoondoka kwenye Maisha yako kinatengeneza nafasi iliyowazi kwa ajili ya vitu vingine bora Zaidi.

Unapofanya biashara ukafeli au ukapata hasara siku zote kumbuka kwamba kuna nafasi ya kujaribu tena. Kuanguka kwako kusiwe ni mwisho bali mwanzo wa kuanza kingine na kukifanya kwa ubora Zaidi.

Business opportunities are like buses, there’s always another one coming. – Richard Branson

Richard Branson aliwahi kusema kuwa fursa za biashara ni kama mabasi ukiona limekupita moja basi kuna jingine linakuja. Usikubali kuaminishwa kwamba fursa Fulani ndio nzuri kuliko nyingine na ukiikosa basi hutafanikiwa tena.

Usikubali kuona kwamba ukipoteza kitu Fulani Maisha yako yote yataharibika. Jua kabisa kinapoondoka kitu inakuwa ni nafasi ya kitu kingine kuja kwenye Maisha yako.

Kila mahali penye matatizo kuna fursa za biashara. Kila sehemu yenye ugumu kuna fursa ya biashara, kila siku kuna watu wanawaza ni namna gani watayafanya Maisha ya wanadamu yaweza marahisi Zaidi. Hivyo ni kwamba kila siku kuna fursa mpya zinakuja kwenye Maisha yako.

Jacob Mushi

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading