KONA YA BIASHARA: Unaona Nini?

jacobmushi
2 Min Read

Chochote unachokifanya sasa hivi kwenye biashara yako lazima kiwe kinafuata ile picha kubwa uliyokuwa unaijenga wakati unaanza. Usikubali kutoka nje ya picha ile hata kama mambo yanakwenda magumu sana. Endelea kuitazama ile picha ikupe hamasa Zaidi.

Unapopitia magumu huwa unaona nini? Watu wengi huona kushindwa, kufilisika, kuanguka kibiashara, lakini leo nataka ubadili namna unavyoona wakati unapopitia magumu yeyote. Badilisha muono wako ona mambo mazuri yanakuja baada ya magumu unayopitia. Ona ukipanda viwango vya juu baada ya magumu unayopitia. Unkuwa kile unachoona na kuamini.

Unaona nini mambo yanapokuwa mazuri? Wengi mambo yanapokuwa mazuri huwezi kuanza kujisahau na kuwa wa kawaida. Napenda nikwambie hapo ulipo sio hapo ulikuwa unataka kufika hivyo usijisahau jiandae kwa kupanda hatua nyingi kubwa Zaidi. Jiandae kwa kupimwa unapotoka hatua uliyopo kwenda nyingine.

Kwenye safari ya mafanikio yako ya kibiashara kuna vipindi vingi utapitia ambavyo vinakuwa kama kipimo cha kuona je upo tayari kufika mbali? Upo tayari kuendelea kufikia kile unachokitaka?

Wakati sahihi wa kujua kama wewe kweli umejitoa kwa ajili ya mafanikio ni wakati mambo yanapokuwa magumu. Unajua wakati mambo yanapokuwa marahisi ni rahisi sana kusema upo tayari na kuongea sana. Lakini yanapokuwa magumu ndio wakati mzuri wa kujua kama yale uliyokuwa unasema ulikuwa unamaanisha.

Tunaweza kujua umejitoa kiasi gani kwenye biashara yako pale changamoto zinapokuwa nyingi. Wengi magumu yanapokuja badala ya kupambana hufunga virago na kwenda nyumbani. Lakini ukweli ni kwamba wakati hasa wa kupambana ni wakati wa magumu. Wakati wa kutafuta mwangaza ni wakati kuna giza. Sasa wengi badala ya kutafuta njia wanarudi nyuma.

Endelea mbele, tafuta namna ya kutoka hapo ulipokwama badala ya kurudi nyuma. Hakuna ugumu unaokuja ambao umezidi uwezo wako.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading