Jinsi ya Kuishinda Tabia ya Kuahirisha mambo.

jacobmushi
3 Min Read

Tabia moja ambayo inawarudisha wengi nyuma ni tabia ya kuahirisha mambo. Na kuahirisha ipo karibia kila sehemu kuajiriwa, kujiajiri, mambo yako binafsi, karibia kila mahali tabia hii inaingia na imewasababishia watu wengi sana wabaki vile walivyo kwa sababu ya kuahirisha.


Umekutana na fursa nzuri sana ikakuhamasisha ukirudi nyumbani yanaanza kukujia mawazo “kwanza sio lazima nianze leo” “nitafanya tu siku nyingine” “Nikiwa tayari nitaanza” hapo ukisema hivyo ujue hutakaa uanze milele labda uje ukutane na hamasa nyingene tena.

Embu jiulize ni mambo mangapi ulisema utayaanza na hadi leo umeanza mangapi? ni kazi ngapi umeziahirisha na hadi sasa zinakusumbua? Ulisema utaacha tabia Fulani leo umefikia wapi?
Dawa ya kumaliza kabisa tabia hii ni kufanya kama ni fursa umekutana nayo ianze mapema iwezekanavyo na usijiulize huna nini angalia ulicho nacho kinawezaje kukupa sapoti ya kuanza. Kama ni kazi zako anza zile kazi ngumu na zinazokupa uvivu maana utaziahirisha tena. 

Tabia hii imekua chanzo cha watu wengi kubaki vile walivyo na kutokuendelea  mbele kabisa. Tabia hii imewasababisha wengi kuja kujuta kwa fursa walizokutana nazo wakaahirisha kisha wanakuja kukuta wengine wamezifanya na wakafanikiwa. 
Unakuta mtu amepata wazo zuri la biashara anasema nitaanza, nitaanza, baada ya muda Fulani unakuja kukuta kuna mtu mwingine alipata wazo kama lako akalifanyia kazi haraka na likamnufaisha ukija kushtuka wewe unakumbuka “hili wazo nilikuaga nalo” umechelewa na wenzako wameshanufaika.

Yapo mambo mengine ukichelewa bado unaweza kuyafanya tena hata leo na ukapata manufaa vile vile lakini muda ulioupoteza hautarudi kamwe kua makini na fursa unazokutana nazo huwezi jua ndio sehemu utatoka kimaisha fanya maamuzi sahihi anza mapema acha kuahirisha.

Zoezi la kufanya:
Andika mambo yote, fursa zote  ulizowahi kukutana nazo na ukaaihirisha kuchukua hatua.

Tafakari endapo ungechukua hatua ungekua wapi leo.


Chambua yale ambayo bado una nafasi ya kuyafanya tena.


Chagua ambayo utaanza kufanya sasa.


Kiasha tuwasiliane kwenye email na simu hapo chini. 

Ukikutana na fursa yeyote hata kama huna pesa huna chochote andika chini faida za wewe kuanza mapema na hasara za kuchelewa kuanza kuna vitu vingine vikishapita havirudi utabaki unajuta tu ningejua ningefanya.

Asante sana na Karibu
Jacob Mushi 

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading