Kama unafikiri kutafuta pesa ni ngumu basi jaribu kukaa bila pesa uone ilivyo rahisi.

Naomba nikwambie Rafiki mafanikio sio lelemama yaani sio kitu ambacho kinakuja chenyewe tu lazima uweke juhudi za kutosha. Lazima uwe na nidhamu ya kutosha.

Wewe usifikiri ni kama vile ambavyo umeshajizoesha. Kuna vitu vya ziada ambavyo unatakiwa kuvifanya na hujazoea kuvifanya na wakati mwingine inawezekana usipende kabisa kuvifanya. Sio vitu vibaya lakini ni vitu ambavyo watu wavivu na waliozoea kujilegeza watachoka haraka.

Nikwambie ukweli nimeanza kuandika tangu mwaka 2015 nimeona watu wengi sana wanakuja na hamasa kubwa lakini wakishaanza kidogo tu wanakata tamaa. Wakishakutana na yale mambo ambayo hwakuyazoea kuyafanya wanarudi katika hali zao za kawaida.

Naomba nikwambie tena Rafiki weka chaguzi mbili tu kwenye Maisha yako ili uweze kufanikiwa. Ili uweze kufikia malengo yako katika viwango vya juu kabisa jiwekee chaguzi mbili yaani ni KUFANIKIWA au KUFA. Naamanisha ni wewe utimize ndoto zako au ufe ukiwa unazitimiza usichague kabisa kubaki katika hali ambayo uliyonayo sasa hivi.

Kamwe usikubali kuchagua kuendelea kubakia na hali ambayo uko nayo. Ndio maana nimekwambia kama kutafuta pesa ni ngumu basi jaribu kuchagua ubaki bila pesa uone ilivyo rahisi. Ukweli kuishi bila pesa ni ngumu Zaidi kuliko kutafuta pesa. Kuendelea na Maisha ambayo uko nayo sasa ni hatari Zaidi kwasababu kadiri mabadiliko yanavyokuja kwako wewe hali itakuwa ngumu Zaidi.

Hakuna njia mbadala Rafiki yangu ni wewe kuanza kufanya vitu vilivyo sahihi na uvifanya kwa bidii sana kuliko mtu mwingine yeyote. Chukua hatua sasa utimize maono yako.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading