Bio

Jacob Mushi ni Mwandishi (Author), Kocha wa Mafanikio(Success Coach), na Mjasiriamali.

Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kwa kupitia Kazi Zake Maisha ya wengi yamekuwa bora na kufanikiwa.

Kwa kupitia kazi yake ya Uandishi pekee ameweza Kuwafikia maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kufikia kualikwa kufundisha vijana, pia kualikwa kwenye vipindi vya Redio na Tv mbalimbali hapa nchini.

Ni mwanzilishi wa Usiishie Njiani Academyambayo inawasaidia watu kujitambua, kujua makusudi yao ya kuwepo hai na kutimiza ndoto zao, na pia inaendesha semina na mafunzo mbalimbali kwenye mtandao.