Mara nyingi tumekua tukifurahi sana pale tunapowaeleza watu juu ya vitu tunavyoviwaza  kama binadamu hua anapata hamasa pale anapomueleza kitu mtu na akakikubali bila kukipinga. Sio vibaya kupenda hivyo lakini kwenye ujasiriamali na mawazo ya biashara iko tofauti kidogo. Wazo lako la biashara kila mtu akilikubali na akakuambia kua inawezekana na utafanikiwa wewe kama mjasiriamali unatakiwa upate wasiwasi.

Kwanini upate wasiwasi? Wazo bora la biashara na ambalo unataka likufikishe mbali na liache alama duniani mara nyingi ukiwaeleza watu upinzani lazima uwepo, kwa mfano aliepata wazo la Kutuma pesa kwa njia ya mitandao ya simu Mpesa, Tigo Pesa etc. kwa kawaida wazo kama hili lilipomjia yule mtu wa kwanza kila aliemwabia alimpinga. Lakini kwa sasa kila mtu anatumia njia hiyo kutuma pesa.
Sio vibaya kua na wazo ambalo halijapingwa ila kama wazo lako la biashara kila mtu anaweza kulifanya halina matokeo makubwa. Kama wazo lako la biashara ukimweleza yule mtu wa kawaida kabisa na akakusifia nenda ukalitafakari tena hilo wazo. Na hapa sio wazo la biashara tu hata kwenye vitu tunavyovifanya maeneo ya kazi na sehemu mbalimbali kama unachokiwaza wewe kila mtu anakiweza kukiwaza na kufanya hicho kitu hakina thamani kubwa.
Rafiki yangu akaniambia tusiishie tu kufikiri nje ya box peke yake bali tulichome na hilo box kabisa. Sasa mimi nakwambia unaweza ukafikiri nje ya box ambalo lipo ndani ya kabati na kabati ambayo ipo ndani ya nyumba na wakati mwingine hiyo nyumba itakua na geti. Hivyo basi toka nje ya geti kabisa. Njoo nje uone dunia jinsi inavyokwenda.

Kwa sasa unaweza kuchukua biashara yeyote iliyopo na ukafikiri nje ya nyumba (sio nje ya box tena) na ukafanya mapinduzi makubwa sana. Hutakiwi uje na wazo jipya ndio lilete matokeo makubwa uanweza kuja na biashara ya zamani ukiwa na mawazo mapya ndani yake. Yale mawazo mapya ndio yatakayoleta mapinduzi katika jamii inayokuzunguka.

Chochote kile kinachofanyika sasa hivi unaweza kukichukua ukawaza vizuri na kwa undani Zaidi ukapata wazo bora sana litakaloleta mapinduzi katika jamii wewe kama mjasiriamali hiyo nayo ni fursa jaribu kufikiria Zaidi ya pale walipofikiri wenzako utaleta mabadiliko makubwa sana, jaribu kuiona dunia itakavyokua miaka mitano ijayo kwa wazo lako bora la biashara ambalo kila mtu amelipinga na ulifanyie kazi.

Asante Sana Na Karibu
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading