Habari za leo ndugu msomaji wetu karibu sana tena leo kwa kujifunza pamoja leo tunajifunza jinsi ya kufnya ili uweze kuzitimiza ndoto zako kuna vitu vya muhimu sana vya kufanya ili uweze kufika kule unapopataka tutajifunza pamoja leo karibu sana.
If a man hasn’t discovered something that he will die for,
he isn’t fit to live.
— Martin Luther King, Jr.
Kama mtu hajagundua kitu ambacho atakifanya mpaka kufa kwake,hajatimia bado kwenye kuishi.
Kuna sababu mbili zinazosababisha wewe usipate kile unachokitaka sababu ya kwanza ni kwamba “hujui ni nini unataka” sababu ya pili ni kwamba “hujamaanisha kile unachikitaka” unaweza kua unatamani kitu lakini kama hujadhamiria kukipata na kuweka akili yako yote na nguvu zako zote kwenye hicho kitu huwezi kukipata utaishia njiani tu lazima uwe umedhamiria haswa kwenye kile unachokitaka. Mfano unataka kuwa mwimbaji bora duniani kudhamiria sio kufanya nusu leo unafanya kesho hufanyi mara zimepita wiki mbili hujafanya mazoezi hiyo itakuwa ni ngumu kutimia kwa ndoto yako.
Let others lead small lives, but not you.
Let others argue over small things, but not you.
Let others cry over small hurts, but not you.
Let others leave their future in someone else’s hands, but not you.
— Jim Rohn
Unayo nguvu ya kutengeneza maisha unayoyataka Mungu amekupa akili uwezo wa kufikiri na nguvu ulizo nazo anataka uzitumie kwa faida ya maisha yako wewe na wengine na kwa utukufu wake. Yeye anakutazama umweleze ndoto zako na sio umweleze tu kama tulivyoona makala zilizopita unatakiwa uanze kufanya. Ninaamini ukisikia maneno haya na ukayafanyia kazi utaona matokeo yake katika maisha yako.
Mungu ametupa uwezo wa kuamua ni maisha gani tunayataka. Hivyo basi cha kufanya ni kuandika vyote unavyovitaka maishani mwako. Haijalishi unataka nini wewe andika tafuta kitabu chako kizuri andika ndoto zako zote. Mtu mmoja akaniambia kuwa huwezi kuchukua daftari tu la kawaida uandike huko ndoto yako ya kununua ndege simaanishi ununue kitabu cha gharama namaanisha kile unachokiona wewe ni kizuri andika ndoto zako zisome kila siku. Anza kupata picha ukiwa kwenye gari lako zuri unalolipenda na usiishie hapo tu mwombe Mungu ingia kwenye vitendo ili ufike pale unapopaona. Mtu mmoja akaseama “kama hujui unapokwenda huwezi kupotea” kama huna ndoto wala malengo ya maisha yake huwezi kusema nimeweza kufanya kitu fulani au sijaweza kufanya kitu fulani.
Soma ndoto/malengo yako kila siku ukiamka kabla hujafanya chochote hujashika simu soma jitazame utakavyokuwa miaka kadhaa ijayo. Mwezi uliopita nikiwa napitia facts mbalimbali nikakutana na fact moja inasema kuwa” vijana wengi hiki wa kizazi wakiamka kitu cha kwanza huangalia simu zao” yaani mtu akifungua macho kitu cha kwanza anatafuta simu iko wapi si vibaya unaweza kutafuta simu ili utazame muda pia. Lakini kitu cha muhimu ni malengo yako kwani hiyo ndio dira na ramani ya maisha yako ndio mwelekeo wa kule unapolelekea pia usisahau mueleze Mungu.
”By writing down your dreams, you open yourself to life’s river
of abundance. But when you read what you wrote down
daily, you multiply the power of that river tenfold.”-Bo Sanchenz
Weka bidii kwenye ndoto zako ukiweka bidii kwenye mambo yasiyo na maana katika maisha yakoa yatakuja kwa wingi. Nakushauri uweke bidii kwenye mambo yote ya msingi amabyo yanahusika katika kutimiza ndoto zako utayaona mafanikio.
Asante sana kwa kujifunza pamoja na mimi tukutane tena kesho.
Imeandikwa na Jacob Mushi 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading