YKULA KIAPO CHA KUTIMIZA NDOTO NA MALENGO YAKO.

Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu natumaini unaendelea vyema katika mipango ya maisha yako

Leo tunaenda kujifunza ni nini cha kufanya ili uweze kutimiza ndoto zako karibu sana  ili tuendelee kujifunza pamoja.

Kama tunavyojua kua mwanadamu ana tabia ya kuchoka  na kukata tamaa mapema leo ninakwenda kukushirikisha njia hii ambayo mimi nimeitumia na nikaona matokeo yake katika maisha yangu.

Kama nilivyotangulia kusema kwenye kichwa cha makala hii KULA KIAPO CHA KUTIMIZA NDOTO ZAKO  ni kwamba unahitaji kujiwekea kiapo juu ya malengo na ndoto ulizojiwekea  kama tunavyojua kiapo huwezi kukivunja ni kama mwanajeshi anapishwa kutimiza majukumu yake. Rais anapoapishwa husema nitaitunza na kuitetea katiba ya nchi hii. Wewe unatakiwa ule kiapo cha kutunza na kutimiza ndoto na malengo yako.

Unahitaji kanuni ambazo hutazivunja na ukizivinja ujue ni majuto kwa maana unaelekea sehemu isiyo sahihi maisha yako. Kanuni ambazo hakuna rafiki, mke, ndugu au yeyote anaeweza kukubadilishia .

Embu jiulize ni wapi ambapo utaenda usikute kanuni na sheria za kuongoza kama ni nyumbani kwenu ulipokua mdogo uliwekewa kanuni na ukizivunja unachapwa viboko. Ulipoenda shuleni ukakutana na kanuni na sheria za shule nazo ukizivunja ni adhabu. Umeajiriwa pia kazini mwajiri kakupa sheria na kanuni zake ukivunja huna kazi. Sasa umebaki wewe tu huna kanuni zako mwenyewe.

Jaribu leo kuweka kiapo cha kutimiza ndoto zako pia weka kanuni ambazo utazifuata nakuhakikishia utaona matokeo makubwa sasa. 

Robin Sharma anasema “One of the greatest regrets a person can ever have is getting to the end of their lives and realizing they did not do their dreams” yaani mojawapo ya majuto makubwa kabisa mtu atakua nayo ni kufika mwisho wa maisha yake na kugundua kua hajatimiza ndoto zake.

Asante sana natumaini umejifunza kitu Makala hii imeandikwa na Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading