Imekuwa ni kawaida sana kila Tunapouanza mwaka mpya kila mmoja hukimbizana na kupanga malengo ya mwaka mpya.

Kuna wanaojua kupanga vizuri sana, kuna ambao hawajui hata kupanga wanaishia tu kusema, kuna wale wanapanga waandika lakini mwezi wa pili ukifika ukiwauliza waliandika wapi hawajui tena.

Wewe binafsi unajijua upo kundi gani, yote hayo ni mazuri kabisa ni hatua nzuri hiyo kujua unachokitaka kuliko yule ambaye anasema liwalo na liwe.

Kazi Kubwa haipo kwenye kupanga kwasababu ni somo ambalo utaelekezwa kwa lisaa limoja tu na utaweza kupanga.

Kazi kubwa ipo kwenye utekelezaji wa kile ulichokipanga.

Kwenye utekelezaji ndipo kuna changamoto.

Kuna kupingwa.

Kuna Kuchoka, kukata tamaa, kukosa hamasa n.k.

Ni wachache wanaoweza kutimiza malengo yao kwa viwango vya juu kwasababu wanaweza kuhimili mikiki ya changamoto.

Nikupe mfano mmoja, ulipokuwa shuleni kuna wale wanafunzi walikuwa wanafauli sana yaani tano bora. Siku zote hawa wanafunzi hata kama kusipokuwa na mwalimu lazima wataendelea kufaulu.

Soma: Uwekezaji Unaolipa.

Lakini ni ngumu sana wale waliobakia kufaulu kwa viwango vyao vya kawaida tu bila ya mwalimu. Na hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo unaweza kuzijua.

Kwenye yale uliyopanga kuna vingi unahitaji msaada. Unahitaji msaada kwenye vile vitu ambavyo ulikuwa unakwama mara kwa mara.

Kinachokufanya usiendelee mbele ni kujiona wewe mwenyewe unaweza. Ukweli ni kwamba unahitaji mtu wa kukusimamia.

Bahati mbaya sana kwenye maisha sio shule, ukifeli hakuna wakukuuliza, hakuna aliekulipia ada ya maisha, hakuna atakaekuchapa viboko. Utajiadhibu mwenyewe kwa kujilaumu na kujiona wewe huwezi chochote.

Kama wewe unafahamu kabisa una tatizo la kushindwa kuweka akiba, yaani mpaka tunavyoongea sasa ikitokea umeumwa ghafla pesa unakwenda kukopa. Basi nakukaribisha sana kwenye Program niliyoandaa kwa ajili ya kukusaidia.

Tuma neno WEKEZA kwenye wasap namba 0654 72 66 68 nitakupa maelekeza zaidi.

Karibu Sana

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading