Kama Unaogopa hatari, hasara, kupoteza, hautakaa uweze kutoka hapo ulipo. Hautawezw kusogea mbele. Maisha ni kujitoa na kufanya bila kuogopa chochote bila kuogopa changamoto.

Kuna vitu huwezi kuvizuia kutokea katika maisha yako na kuna ambavyo unaweza kuvizuia. Usivyoweza kuvizuia Achana navyo wala usivipe nafasi ya kukuzuia wewe kufanya jambo. Jinsi unavyozidi kusita kufanya maamuzi ndivyo unavyozidi kupoteza muda.

Hua napenda kujifunza kwa watu wanaofanya mambo ya kutisha yale mambo yanayoweka maisha yao hatarini.

Wachimba madini:
Hawa ni Mojawapo ya watu waliosema hatuogopi chochote hatuogopi kufukiwa na kifusi hatuogopi kukosa hewa. Tunachotaka ni kupata madini. Japo kila wakati unasikia wengine wamefukiwa na vifusi, wengine wamekosa hewa wakapoteza maisha bado kuna wanaoingia kuchimba kila siku.

Wewe ni kitu gani hasa kinakupa hofu na Unaogopa kufanya biashara au kuchukua hatua? Ni kifo? Kitu gani cha muhimu kama UHAI? Wewe Unaogopa kupata hasara ya pesa? Mafanikio sio rahisi hivyo, lazima ukubali Lolote litakalotokea nipo Tayari kupambana nalo.

Wanajeshi:
Hawa ni watu wengine ambao nawaheshimu sana. Watu waliotoa maisha yao kwa ajili ya wengine. Yaani wapo Tayari kufa ili kukutetea wewe mwananchi. Sio kitu cha kawaida kabisa mtu unaenda vitani unajua kabisa hapa kufa kupo yaani kufa ni kitu cha kawaida tu. Watu wametoa uhai wao kwa ajili ya wengine bila kuogopa bila kuwaza familia zao. Wake zao watoto wao.

Lakini wewe Unaogopa kupoteza pesa yako Unaogopa kupata hasara. Utajiri haupatikani kirahisi hivyo yale maisha unayotaka hayaji kirahisi hivyo. Ili utoke hapo ulipo lazima uwe Tayari kwa Lolote kubali kwamba hasara hua zipo kama. Mchimba madini anavyofukiwa na kifusi au kama mwanajeshi anavyopigwa bomu na kufia vitani.

Acha woga. Tanzania inahitaji watu majasiri sana ndio maana unaitwa mJASIRImali.

Changamoto hua zipo tu usiogope kabisa.
Fanya maamuzi haraka chukua hatua maisha yako Hayatakua kama yalivyokua.

Karibu sana
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading