Kuwa wa Kipekee maana wewe ni wa Pekee

jacobmushi
2 Min Read

Habari ya leo ndugu msomaji wetu mzuri ni matumaini yetu kuwa unaendelea vyema na maisha yako. Karibu tuanze week end kwa kujifunza pamoja.
Kuwa wa kipekee maana wewe ni wa pekee. Tunasema wewe ni wa pekee maana hakuna mwingine kama ww huku duniani hata kama mnafana sura na majina. Wewe unayo nafsi yako peke yako na haifanani na mwingine. Kisayansi tunasema kila mtu ana DNA yake ya peke yake alama za vidole nazo hazifanani. Hata namna ya kufikiri tunatofautiana.
Kitu cha ajabu ni kwamba unakuta mtu anataka kuwa kama fulani kwa kuiga namna anavyoishi anavyoongea na vingine vingi. Ukitambua kua wewe ni wa pekee utafanya mambo ya kipekee. Sio vibaya kujifunza kwa wengine ila ni vibaya kucopy jinsi ya kuishi.
Wewe ni muimbaji imba kipekee lakini jifunze kwa waimbaji wenzako. Muigizaji igiza kipekee usijaribu kuigiza kama fulani hutaweza. Mwanasiasa fanya kipekee usiige mtu. Utakuwa unajipoteza wewe mwenyewe unaishi maisha ya mtu mwingine.
Hatukuja duniani kushindana nani kafanya zaidi ya nani wala usipofanya hutaulizwa na mtu labda kama wewe bado ni mtoto. Unachotakiwa kujua wewe ni sababu ya wewe kuwepo duniani hadi leo na uitumie hiyo nafasi ya kipekee kufanya jambo hilo kwa kipekee zaidi.
Embu jiulize simu ya Samsung wangeiga jinsi Iphone wanavyofanya wangefika mbali? Kwanza wasingeweza kuiga wangeachwa nyuma tu. Hata wewe huwezi kuishi kwa kuiga fanya kila jambo kwa kipekee hata kama linafanana na la mwenzako lakini upekee ndio utakaotofautisha wewe na huyo mwenzako.
Asanteni kwa kujifunza nami naamini hata week end hii utaimaliza vyema kwa namna ya kipekee lakini iwe na manufaa katika maisha yako.
Imeandikwa na Jacob Mushi. 
0654726668
mushijcob@gmail.com
Karibu sana.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading