Jijengee Tabia ya Kuweka Akiba.

jacobmushi
3 Min Read

Habari rafiki, hongera kwa kuchukua hatua ya kutaka kujijengea tabia ya kuweka akiba. Hii ni tabia ambayo watu wachache sana wanayo na imewawezesha kuishi maisha ya mafanikio yasiyo na hofu.

Embu jiulize kama sasa hivi ungekuwa na akiba ya fedha ambayo inatosha kuendesha maisha yako hata kama hufanyi kazi yoyote kwa miaka 5 ungeishi kwa mashaka? Ikitokea umefukuzwa kazi unaweza kupata presha? ikitokea nyumba unayokaa imevunjwa unaweza kuanguka kwa hofu? Jibu ni hapana kwasababu unazo pesa za kukuinua unapopata majanga ya aina yoyote.

Sasa usitake kuanza nja makuu, chagua kiasi ambacho wewe binafsi unaweza kuanza nacho, au kwa ushauri ni hakikisha unaweka angalau asilimia kumi ya kipato chako. Kama unapata laki kwa mwezi basi weka akiba tsh elfu kumi.

Naomba uangalie mfano huu hapa:

Mwaka 1 Una Siku 365.

Kwahiyo Mwaka Huu KAMA Kila Siku Ukiweza 

Kuhifadhi (Save) Tsh 1000/= (elfu moja) kila siku MWISHO WA MWAKA Utakuwa Na Tsh 365,000/= (laki tatu sitini na tano elfu)

UKIHifadhi (save) Tsh 2000/= (elfu mbili) kila siku MWISHO WA MWAKA Utakuwa na Tsh 730,000/= (laki sab ana thelathini elfu)

UKIhifadhi (save) Tsh 5000/= (elfu tano) kila siku MWISHO WA MWAKA Utakuwa na 1,825,000/= (milioni moja laki nane na ishirini na tano elfu)

Ukihifadhi (Save) tsh 10,000/= (elfu kumi) kila siku MWISHO WA MWAKA Utakuwa na 3,650,000/= (MILIONI TATU LAKI SITA NA ELFU HAMSINI)

Wote tunakubaliana kwamba haya ni mahesabu rahisi sana na kama mtu anapata kipato katika hiyo mifano hapo kuna ambao anaweza kumudu. Lakini cha kushangaza sasa bado wewe hujaweza kufanya hivi na hata ukiweza basi utakuja kusikia mwisho wa mwaka hujui uliishiaga wapi na mpango wako.

Sasa mimi nimeliona tatizo liko wapi, tatizo kwamba huna msimamizi, huna mtu wa kukumbushia kila wakati yale malengo yako. Na hii inawezekana ni kwasababu ya mambo mengi uliyonayo. Sasa mimi nimemeamua kujitoa kwa ajili ya nafasi hiyo ya kukukumbusha Rafiki.

Ili uweze kuwa na tabia hii nimejitolea kukusaidia kufuatilia na kuhakikisha umeweka akiba. Wewe utachagua unataka kuweka akiba kwa mwezi, kila wiki, au kila siku kulingana na aina ya kipato chako.

Utalipia Ada kila mwezi ya kuongozwa na kufundishwa kujenga tabia hii. Ada ni Tsh 10,000/= (elfu kumi tu kwa mwezi). Ada hii utakuwa unailipa kwenye tarehe ile uliyoanza program hii.

Kama upo tayari basi nitumie ujumbe AKIBA kwenye namba 0654 726668 WhatsApp Nikupe maelekezo yote.

BONYEZA MANENO HAYA KUTUMA UJUMBE WHATSAPP

Karibu sana

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
4 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading