KWANINI BINADAMU HATUWEZI KUFANANA KIFIKRA?

Maisha yako ni shule ambayo wengine watakuja kujifunza siku sio nyingi.
Ulivyoishi maisha yako ndio itaamua uwe shule ya watu wengi kiasi gani.
Kila ambacho unakifanya kila siku jiulize unakuja kuacha darasa la namna gani kwa wengine?
Ukitenda mabaya utakuwa mfano mbaya, ukiweza kufikia ushindi wako utakuwa mfano wa kuigwa.
 Moja ya jukumu unalopaswa kujipa kilasiku ni kuhakikisha una furaha bila ya kujali ni mambo gani unapitia.

 Wakati wowote unapogundua kuwa hakuna mtu anaekujalu wala kuonyesha kuguswa na mambo yako ndio wakati haswa unaopaswa kujijali, kujipenda na kujiombea kuliko wakati mwingine wowote.
Unapofika wakati ukaona hakuna wa kumweleza yale unayopitia huo ndio muda unapaswa utambue kuwa yupo Mungu awezae yote na msikilizaji wa matatizo yako.
 Tengeneza desturi/utaratibu wa maisha yako ambao utaufuata kila siku unaoendana na maono yako. Huwezi kufika popote kama hakuna vitu ulivyoamua kuvifanya mpaka vilete matokeo ya kule unapopaona, huwezi kufika mahali kama kuna mambo bado hujaamua kuyaacha.Ukubwa wa matokeo ni ukubwa wa maumivu aliyopata mtengeneza matokeo. Unapofurahia matokeo fulani jua kuna mtu kaumia na kutoka jasho.
Usimdanganye mtu yeyote kuwa huwezi kuishi bila yeye, ukweli ni kwamba unaweza kabisa kuishi bila mtu yeyote hapa duniani na pia unaweza kuishi na watu wengine hata huyo akiondoka.
Hatuwezi kuishi kama tutafikiri kwa namna moja, maisha yangekuwa magumu sana. Kila mmoja ana namna yake ya kufikiri na kutenda.
Wanyama peke ndio wana mlingano mmoja wa kufikiri ndio maana huwezi kukutana na mnyama aliepiga hatua zaidi ya wenzake.
Hatuwezi kuishi maisha ya kukubaliana kwa kila jambo.
Kila linalosemwa unakubali.
Ukiona upo hivyo ujue wewe huna uwezo wa kufikiri tofauti au kuleta changamoto kwenye mawazo ya wengine.
Kuna watu waliweza kufanya mambo makubwa kwasababu tu kuna watu waliwaambia huwezi.
Kuna watu wameleta mabadiliko makubwa kwenye jamii kwasababu ya kupishana mawazo na wengine.
Huhitaji kuacha unachokifanya na kuanza kupambana na anaekupinga, unapaswa kuendelea mbele kufanya hadi yale asemayo yashindwe.
: Wakati wewe unafurahia kununua nyanya kwa bei ya chini kumbuka kuna mtu analia ameuza kwa hasara.
Wakati unalia bei imepanda kuna mtu anafurahi amepiga hela nyingi kwa mzigo aliotoa shamba.
Ni muhimu kujua kwamba karibu kila unachokifurahia kuna mwingine amepata maumivu japo sio kwenye kila kitu.
Ukitambua hilo hutaweza kuwa mtu wa lawama kwenye kila jambo.
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI 2018

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading