Habari za leo msomaji wetu ni matumaini yangu unaendelea vyema na harakati za kutafuta mafanikio. Leo tunakwenda kujifunza sababu za muhimu wewe kufanikiwa.karibu sana tujifunze pamoja.

Pesa sio kitu cha muhimu sana duniani lakini inagusa sehemu nyingi za muhimu katika maisha yetu hapa duniani.

Mungu anawapenda maskini kwa sababu anataka watoke kwenye umaskini wao na sio kwamba  wabaki na huo umaskini.

Kama unataka mafanikio/utajiri wan chi yako anza wewe binafsi kufanikiwa kuwa tajiri na maendeleo kwanza wengine watafuata nyuma yako.

Ili uweze kuwasaidia wengine kwenye maisha yao inabidi wewe uanze kujisaidia mwenyewe kwanza.
Usipojipenda wewe huwezi kumpenda mtu mwingine.
 
Watu wanabakia masikini wakidhani hiyo ni adhabu Mungu amewapa. Lakini kama ambavyo wewe unaumia kumuona mtoto wako akipitia mateso ndivyo Mungu wetu anaumia kutuona sisi ni maskini. Na ni kwamba yeye haweza kukuletea utajiri kama muujiza ni lazima ufuate kanuni zote za utajiri na mafanikio kanuni ya kwanza ni kutambua kuwa wewe unajukumu gani hapa duniani.

Usitegemee Mungu atafanya kila unalolitaka wewe nikiwa na maana kuwa sio kila utakachoomba kwa Mungu utajibiwa vingine hujibiwi kwa sababu unatakiwa utumie akili yako kufikiri Mungu amekupa akili na maarifa kwa hiyo ni lazima uzitumie. Wakati mwingine unamwomba Mungu jambo ambalo wewe uitakiwa ufanye na anajua unaweza kulifanya hawezi kukujibu atakusubiria ufanye wewe. Tafakari ni mambo mangapi umemwomba Mungu na unasubiri akujibu yeye anasema ( hachelewi wala hawahi anajibu kwa wakati wake) kumbe wewe unamsubiri nay eye anakusubiria ufanye. Mimi ninakuambia fanya yeye yupo pamoja na wewe. Soma mithali 40:4

Imani bila matendo imekufa kama una amini wewe ni tajiri, una amini Mungu atakubariki, una amini Mungu  atayajibu maombi yako na hufanyi matendo yeyote kuelekea kwenye kile unachokiamini basi imani yako imekufa na kile unachokiamini hakina maana hakina maana kwa kua imani bila matendo imekufa. Anza sasa kufanya yale unayoyaamini usimsubiri Mungu akujibu atakujibu ukiwa umeanza kufanya. Wakati unamsubiri Mungu afanye kitu kwenye maisha yako na Mungu anakusubiri wewe ufanye ili akusaidie.

Kama tulivyoona kwenye makala iliyopita kuwa muujiza uanousubiria ni wewe pia vilevile ili ubarikiwe ili upokee muujiza lazima uhusike katika kuusababisha muujiza utokee maishani mwako soma 1Thethalonike 4:11-12.

Mungu ametuumba sisi tufanye kazi na kumuamini yeye na sio tu kumuamini yeye pekee. Jitahidi uwe mwanadamu bora na wa thamani ili umtukuze yeye aliekuumba.

   Asante sana kwa kufuatana nami tukutane tena kesho kwenye makala         nyingine. 
  Imeandikwa na Jacob Mushi 0654726668 mushijcob@gmail.com
 Tembelea ukurasa wetu wa Facebook Rise and Shine Tz

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading