HATUA YA 389: KWANINI UNATAKIWA UMJENGEE MWANAO MTAZAMO HUU?

jacobmushi
3 Min Read

“Kile Unachokijua Kinakuathiri Sana Kuliko Unavyofikiri.”

Nilipokuwa mdogo mtu mwenye mafanikio sana niliekuwa na mfahamu alikuwa anafanya kazi ya udereva. Hivyo nikawa nikiamini kwamba nikiwa Dereva na mimi nitakuwa na mafanikio. Niliendelea kuamini hivyo hadi nimefika darasa la saba. Hali hii ilisababisha mpaka wale ambao wananisomesha waliponiuliza unataka kuja kuwa nani nikawaambia nataka kuja kuwa Dereva.

Wengi walishaangaa huyu mtoto ni wa aina gani, lakini yote haya yalisababishwa na mimi kuwa na taarifa kwenye akili yangu kwamba mtu mwenye mafanikio ni Dereva. Niliendelea kuamini hivyo mpaka pale nilipokutana na wengine ambao wamefanikiwa kwenye kazi zao nyingine.

Nakumbuka pia niliwahi kuambiwa nenda kasomee ualimu kwasababu ndio kazi yenye uhakika yaani wewe ukimaliza kusoma tu una kazi yako unaanza kula mshahara.

Nilipoanza kusoma Vitabu ndio niligundua kwamba kuna mambo mengi mno nilikuwa siyajui. Nikaanza kuwafahamu wajasiriamali matajiri, waandishi, wazungumzaji, wagunduzi wa vitu mbalimbali na viongozi wenye mafanikio makubwa.

Nikaanza kupata mwangaza mpya, nikaanza kuona upya Maisha yangu katika picha nyingine ya tofauti kabisa. Nikaanza kugundua vile vitu nilivyokuwa navifanya nikiwa mdogo bila kujua ni nini nafanya.

Kile ambacho ulianza kukifahamu ukiwa mdogo kitaendelea kukutesa mpaka pale ambapo utakibomoa na kuanza kujifunza vitu vingine vipya ndani ya akili yako. Sio rahisi ukubaliane na hiki kwasababu ni Imani hiyo umeijenga tangu ukiwa mtoto.

Nataka ujiulize maswali kwanini mwanao amechagua kile ambacho anasema anataka kuja kuwa? Inawezekana sio kitu anachokipenda ila ni kwasababu tu ndani ya akili yake taarifa aliyonayo ni ya daktarin aliena mafanikio au Maisha mazuri. Inawezekana aliambiwa ukiwa injinia utakuwa na Maisha mazuri.

Mpe nafasi mwanao ajue mambo mbalimbali hata yale ambayo hakwendi kujibia mtihani shule. Mpe nafasi afahamu mambo yatakayomsaidia siku atakapokuwa kijana mwenye ufahamu. Kuna siku mawazo yake hayo unayomwambia yatakuja kumuathiri sana na wewe hutakuwepo.

Ni kweli hawezi kufahamu kila kitu ila kuna mambo ambayo anaweza kuyafahamu na yakamsaidia sana kwenye Maisha yake yote. Mpe nafasi ya kujua mambo mengine mengi Zaidi kuliko yale ya shuleni tu kwasababu yatamsaidia katika kufanya maamuzi sahihi wakati atakapokuwa na ufahamu wa kiutu uzima.

Mwambie kwamba hata yeye anaweza kuja kuwa bilionea kwenye umri wake wa ujana. Mwonyeshe watu ambao wameweza kufanya mambo makubwa sana wakiwa na umri mdogo. Hii itamjengea ufahamu wa inawezekana.

Nikukumbushe, umeshajiunga na program ya Coaching? Nafasi ni chache Kujiunga Bonyeza Hapa >>> https://goo.gl/gWbh7K

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading