520; HEKIMA: Kwanini Wengine Wanashinda?

By | January 19, 2020

Ni kwasababu wameamua kulipa gharama,

Ni Kwasababu wameamua kujitoa kwa kila namna,

Ni kwasababu wameamua na wapo tayari kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza.

Ni kwasababu wamebadili mitazamo yao kutoka vile walivyokuwa mwanzo na sasa wana mitazamo kama wale waliofika mbali zaidi.

Ni ukweli huo rafiki kama haupo tayari kulipa gharama huwezi kupata kile unachokitaka.

Kama hujaamua kuweka muda wa kufanya mazoezi misuli haiwezi kutokea yenyewe.

Kama kila siku umekuwa mtu wa kuongea tu bila ya vitendo kamwe huwezi kupata majibu ya maisha yako.

Hivi unajua hata maji usipoyatengenezea njia yatakwenda sehemu ambazo hayakutakiwa kwenda? Hivyo ndivyo na maisha yako yalivyo usipoamua kuyatengenezea njia lazima yataelekea sehemu mbovu.

Kwanini sasa wewe mpaka leo umekuwa mtu wa kutoa sababu za kwanini hujafanya hivi au vile. Kwanini sasa usianze kujitengenezea mifereji ambayo itatirisha maji yenyewe kuelekea kule unakotaka?

Kubali kulipa gharama ndugu, kubali kujitoa, kubali kuweka nguvu kubwa, usiwe mtu wa kuongea peke yake.

Nakutakia Kila la Kheri katika Kulipa Gharama.

Kupata huduma mbalimbali ninazotoa tembelea kwenye link hii www.jacobmushi.com/huduma

Rafiki Yako

Kocha Jacob Mushi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *