KWANINI WEWE UPO HAI MPAKA LEO? SOMA HAPA

jacobmushi
2 Min Read
SABABU YA WEWE KUA HAI MPAKA SASA NI HII…
Habari ya leo ndugu msomaji wa mtandao huu. Karibu tena leo kuendelea kujifunza nasi.
Leo tunajifunza sababu ya wewe kua hai mpaka sasa. Embu jiulize ni watu wangapi unaowafahamu wameshafariki lakini wewe upo hai ulishajua kwanini upo hai?  

Leo nitakwambia kwanini bado upo hai. Upo hai kwasababu kuna lile jambo lililokuleta hapa duniani hujalikamilisha.

Hebu juliulize tena ni ajali ngapi zimetokea hapa nchini. Wewe ulisafiri mara ngapi kipindi kile cha mfululizo wa ajali lakn upo hai huna kilema chochote. Sio kwamba umetenda mema sana. Mimi ninakwambia lile jambo lililokuleta hapa duniani hujalikamilisha.
Mimi sijui wewe ulikuja hapa duniani kwa sababu ipi ni jukumu lako na langu kutambua kwanini ulizaliwa na mpaka sasa umeshafanya nini. Ninachoweza kukwambia ni kwamba nafasi bado zipo za wewe kufanikiwa kwa lile unalolifanya usikate tamaa Mungu amekulinda mpaka sasa  kwa sababu ya kusudi hilo lililopo ndani yako. 
Nafasi ya wewe kufanikiwa bado ipo haijajazwa na mtu ndio maana bado upo hai na umeweza kusoma hapa leo.
“Kwakua bado upo hai mpaka leo kuna jambo hujalikamilisha kwenye hii dunia usikate tamaa”
Asante sana kwa kusoma makala hii ni matumaini yangu umejifunza kitu leo.
Imeandikwa na Jacob Mushi
Karibu sana.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading