Habari rafiki yangu. Umeanzaje wiki yako?

Hakuna mtu mwenye siku Zaidi ya moja yaani wote tunaishi kwa siku moja ambayo imebeba masaa 24. Kwa wanoweza kuitumia vyema siku hii moja wameweza kupiga hatua. Kwa walioshia kusema kesho wataanza wmeishia kuendelea kutoa sababu kwanini hawajafanya.

Usikubali kuendelea kuwa mtu wa aina hii fanya kitu leo. Haijalishi ni kidogo kiasi gani unachokifanya kwa mkusanyiko wa miaka unaweza kufikia lengo lako.

Unajua huwezi kuwaajiri wafanyakazi 100 kama hujaweza kuanza na mmoja. Kama mmoja hujaweza kukaa nae vizuri na akafanya kazi sawasawa hao mia moja watakutoa jasho. Anza na huyo mmoja kwanza ujifunze jinsi ya kukaa nae.

Leo unaitumiaje kutimiza ile ndoto yako kubwa. Unajua kabisa haiwezi kutokea kwa siku moja ikatimia lazima kuwepo na hatua unazopiga kila siku. Wingi wa hatua unategemeana na ukubwa wa ndoto yako.

 

Ukiona mwenzako amefikia kule anapokwenda usishangae hujui alipotoka. Hujui alikuwa anafanya nini wakati haonekani. Hujui wakati akiwa ndani anafanya vitu gani. Wewe endelea hakuna haja ya kutaka kuwaonyesha watu na wewe upo kwenye mstari.

Matokeo ya kile unachokifanya yatakuja kukusimamisha mbele za watu. Kuna nyakati unaweza kulazimisha kulazimisha kutambulika na ukaishia kudharaulika lakini ukisubiri matokeo ya kazi yako heshima itakuwa kubwa Zaidi.

 

Nikutakie juma lenye mafanikio.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading