Maamuzi chanya madogo madogo unayofanya kila siku ndio yataamua aina ya Maisha utakayokuja kuishi miaka 5/10/20 ijayo. Fanya maamuzi sahihi, chukua hatua bila kukata tamaa.

Mafanikio sio hatua kubwa Fulani ambayo unatakiwa uifikie ndio tuseme umefanikiwa bali ni matokeo chanya kidogo kidogo ambayo unayapata kila siku kwa hatua unazochukua. Kama kila siku kuna jambo unakuwa umelifanikisha unahesabu hayo ni mafanikio yako kwa siku hiyo.

Hatua ndogo ndogo unazopiga kila siku zinaweza zisionekane na watu wengi sana lakini mkusanyiko wake unaweza kuja kusababisha mabadiliko makubwa sana kwenye Maisha yako.

Unapopanda mbegu moja inatoa mti au shina la zao ulilopanda na unapata matokeo ya mazao mengi sana kwa kupitia mbegu moja uliyootesha. Kwa hatua yeyote uliyochukua leo inaweza kuja kuleta matokeo makubwa ambayo kwa wakati mwingine hukuyatarajia.

Jenga utaratibu wa kuhesabu hatua unazopiga kila siku. Kama ulisema unasoma vitabu kila siku hakikisha unajifanyia tathimini ya kile ulichokisoma.

Kama ulisema utafanya mazoezi hakikisha umefanya na umefikia lengo uliloweka.

Usisubirie matokeo makubwa kwa siku moja badala yake tengeneza tabia ambazo zitakusababisha wewe ubadilike ndani na uvutie mambo makubwa Zaidi.

Huwezi kufanikiwa nje kama hujaanza kufanikiwa ndani. Hii ndio maana tunawahamasisha watu juu ya maendeleo binafsi. Vile ulivyo ndani ndio kunavutia matokeo ya nje.

Usiogope unapoanza hutapata matokeo ya haraka. Unaweza kuona mbona hubadiliki? Mbona umefanya jambo Fulani lakini huoni matokeo? Wewe endelea kufanya kuna tabia ambazo huwezi kuziondoa kwa haraka inachukua muda mrefu kuziondoa kwasababu ilichukua muda mrefu pia kuzitengeneza.

Hakikisha kila siku kuna hatua umepiga kwenye Maisha yako, kwenye mahusiano, kazi yako, na kiroho chako. Jifunze kila siku na fanyia kazi kile unachojifunza.

 

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading