Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema. Leo napenda nizungumze na mabinti ambao wanataka mafanikio. Mafanikio katika maisha na ndoa zao. Tumejifunza sana kuhusu mafanikio tukasema ni lazima uwe na Ndoto kubwa na uziandike kisha uzifanyie kazi. Pia Kwenye upande wa Mahusiano ni muhimu kuwa na Ndoto na malengo.

Moja ya vitu nilivyokuja kuvigundua ni kwamba  wasichana wenye umri kuanzia miaka 25 kurudi chini, wanajisahau sana na kufikiri watabaki kuwa wasichana milele. Hapa wanaweza kuchagua sana, dharau nyingi. Kama huna pesa una mapenzi ya kweli huwezi kupata nafasi Kwao. Wanasahau kwamba huo ndio umri wa kujiandaa na kuwaandaa waume zao. Wanatumia muda mwingi zaidi na waume wa wengine bila kujijua.

Hakuna kitu Kizuri kilichotokea chenyewe,  hakuna mwanaume mwenye mafanikio alieibuka peke yake.  Wengi wameanza chini kabisa wakihamasishwa na kutiwa moyo na wale wawapendao na hatimae kufikia mafanikio. Ukitaka kitu Kizuri hakikisha unajua kukiandaa. Unaweza kumuandaa mume wako kipindi hiki cha umri wako mdogo. Acha kupoteza muda na wavulana wasiojielewa watakuharibia maisha yako. Yeyote anaekutaka kimwili na hajaonyesha ana nini Kwenye maisha yake ya baadae huyo mkimbie.

Badala ya kutumia umri huu kula maisha, kubadili wanaume,  kutembea na waume za watu. Kaa chini mwandike mwanaume unaemtaka. Andika sifa zote, maisha unayotaka awe nayo, nguo unazopenda avae,  na mengine yote.

Siku ukija kumpata hata kama sifa hana unaweza kukaa nae chini ukamwambia akueleze anaona nini kwenye maisha yake. kila kitu kinatengenezwa hata yule mume wa ndoto yako anatengenezwa. Usitegemee kumkuta akiwa tayari vile unavyotaka.

Vile vile tumia muda huu kumuombea hata kama humjui muombee kule aliko Mungu amlinde na wanawake waovu,  roho za uzinzi na tamaa.

Kwanini umwombee?  Kwasababu hujui ni nani na hujui anachokifanya.

Usisubiri hadi umri umeshasogea ndio unaanza kumuomba Mungu.

Kumbuka usichana hautakaa urudi tena muda hautarudi nyuma tena. Ukiweza kutumia vyema muda wako unaweza kumuandaa mume bora na maisha yenu yakawa na furaha milele.

Kamwe usikubali kushusha thamani yako kwa kuvuliwa nguo na kila mwanaume. Haijalishi una uzuri wa aina gani kama wewe kila anaekuita unamkubalia huna thamani. Kitu chochote kinachopatikana kirahisi thamani ipo chini sana. Huo mwili sio wa kila mwanaume. Yupo mmoja ambae ni haki yake kuufunua. Kama wewe unafikiri ni mrembo sana basi ndio unapaswa uwe na uvumilivu na ujitunze zaidi.

Hivi ukiambiwa leo kwamba ulizaliwa ili uje kuwa mke wa Raisi utavua vua nguo hovyo? Huwezi lazima utajitunza lakini wengi mmeshindwa kwasababu hamjui mnapokwenda. Ukijitambua wewe kama binti utajitunza. Amua leo kujitunza mme wako ni bilionea,  Raisi wa nchi, Waziri,  na wengine wakuu unawafahamu.

Usikubali kupiga piga picha za hovyo na kuziweka mitandaoni. Hujui ni nani atakae kuja kukuoa. Embu fikiria kesho umeolewa harusi nzuri sana halafu picha zako za utupu ulizotuma kwa mwanaume fulani zinavuja? Picha ulizopiga sehemu zako za siri zipo wazi umeziweka Instagram kila mwanaume aone!  Wewe ni wa mmoja tu. Kuna picha wanatakiwa waone watu na kuna picha Anatakiwa aone mumeo.

Anza kubadilika sasa.

SOMA : SEHEMU 2 ZA KUZINGATIA WAKATI UNATAFUTA PESA KWA BIDII.

Umri ukisogea akavuka 26-35 hapo ndipo wengi huanza kugundua kwamba muda umeshakwenda. Na mara nyingi hujikuta wanafanya maamuzi bila kufikiri.

Hapa kila binti hutamani kuolewa kuliko kitu kingine. Sasa kama wewe ulishaweka akiba ya maombi,  na pia tayari unajua unachokitaka huwezi kuyumbayumba. Yule Mungu aliekupangia bado yupo na atatokea tu.

Kamwe usikubali kufanya maamuzi kwa haraka bila kufikiri. Unaweza kuja kujuta zaidi.

Mtu mmoja akauliza  “Ukikuta kuna ndizi mbivu zipo sehemu ya wazi sana. Moja imemenywa maganda na nyingine ina maganda yake wewe utachukua ipi?”  Watu wote walijibu kwamba watapenda wale ndizi iliyo na maganda. Kwasababu ile iliyomenywa ni rahisi kuingiliwa na wadudu pamoja na uchafu hivyo sio ndizi salama

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading