Haya ni mambo ya muhimu sana ya kubadilisha la sivyo hali itakua ngumu zaidi kwako.
1. Kutokutendea kazi unayojifunza.
Umejifunza Mambo mengi, umehamasika vya kutosha, usipochukua hatua ya vitendo hali itazidi kuwa ngumu zaidi. Kuna vitabu umesoma, au umeomba ushauri na ukashauriwa lakini unasita kuchukua hatua mwisho wake ni mgumu zaidi.
2. Kuahirisha mambo.
Umeamua kufanya jambo lifanye achana na tabia ya Kuahirisha kila wakati. Umeamua kuanza anza leo waambie watu fanya na matokeo utayaona. Ukitaka hali izidi kuwa ngumu kwako mwaka 2017 endelea Kuahirisha. Umeambiwa kuna semina Nzuri sana ahirisha tu useme zitakuja nyingine.
Hali itazidi kua ngumu mara dufu.
3. Kutokuwa na Malengo na Mipango.
Kama maisha yako unayaendesha bila mipango halafu unaishia kulalamika utegemee nini mwaka 2017? Tegemea magumu zaidi usipobadilika.
Maisha yako yanatakiwa kuwa bora na ni jukumu lako kuyafanya yawe bora, hakuna mtu mwingine atakuja kukusaidia wewe.
Weka Mipango, Malengo na uyafanyie kazi.
Soma: Jinsi Ya Kuanza
4. Kudharau Mafundisho.
Endelea na tabia yako ya Kudharau wanaokuandikia Mafundisho kama haya. Dharau wanaokushauri usome vitabu, Dharau wanaokwambia usikilize audio books. Waone tu kama wanataka kukuondolea starehe yako ya kusoma magazeti yasiyo na mchango wowote kwenye mafanikio yako. Halafu tegemea maisha yawe bora 2017. Huo ni uongo na nitakuwa nakudanganya.
Ukitaka kuwa na maisha ya tofauti anza kuishi maisha ya tofauti kwa kufanya vitu vya tofauti.
5. Kuridhika na Hali uliyonayo.
Wewe una uhakika wa chakula, malazi, na mavazi vile vile Inawezekana una usafiri wako tayari. Itakua ni hatari sana na wewe kuporomoka kama utaridhika na maisha uliyonayo sasa kwani ndio mwanzo wa kupotea.
6. Matumizi mabaya ya Pesa na Muda.
Umekua na matumizi mabaya ya pesa na muda. Kila unachopata unatumia chote. Uko free masaa yote. Kila anaekuja anaweza kukuchukua tu mkaenda kutembea. Halafu utegemee hali yako ibadilike. Nitakuwa nakudanganya rafiki yangu. Ukweli ni huu hali yako itazidi kuwa mbaya sana.
Kwenye picha anaonekana tajiri wa kwanza wa Dunia na mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bwana Bill Gates. Ni mzee, halafu ana pesa inayoeleweka. Pili kama ni historia yeye ameshaacha. Kama ni kusudi tunaweza kusema ameshalitimiza. Kama ni uvumbuzi amebadili dunia kwa kiwango kikubwa sana.
Lakini kuna kitu ameshika mkononi mwake. Ni vitabu ameshika anajifunza nini? Yeye si alipaswa akacheze golf? Si ameshafanya kila kitu?
Lakini anajifunza, kujifunza hakuna mwisho. Leo kwa kupitia semina na vitabu unaweza kugundua kitu kipya na kikaleta mapinduzi kwenye maisha yako na duniani.
Usisahau kujipatia kitabu kiitwacho Siri 7 Za Kuwa Hai Leo
Jacob Mushi
Trainer, Entrepreneur & Author.
Phone : 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com