Habari za leo mpendwa Rafiki msomaji, ni matumaini yangu unaendelea vyema sana na majukumu yako kila siku. Leo katika kipengele cha mafanikio tunakwenda kuangalia mambo ambayo yanaweza kua sababu ya wewe kupoteza kila ulichonacho kama usipoyarekebisha. Karibu ujifunze nami.

Mara nyingi wengi wakishapata mafanikio makubwa hujikuta wanamsahau Mungu na kudharau hata wale waliokua wakiwaombea. Kama kuna kitu cha kwanza kitakufanya upoteze kila ulichonacho na ni kumsahau Mungu mwanzilishi wa vyote. Unapomsahau kwanza unakosa ulinzi, ulinzi ukikosekana ni rahisi adui kukushambulia na kufanya vyote ulivyonavyo vipotee. Unapoteza nguvu ulizonazo au kutumiwa vibaya na shetani. Ni kweli binadamu wote tumezaliwa na nguvu kubwa sana ndani yetu lakini unapokosa uongozi wa yule alieziweka lazima zitumike kinyume. Kua makini sana usije ukamsahau Mungu tukakusahau. Biblia inasema katika kitabu cha Mhubiri, Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako. Hivyo katika kila hatua ya mafanikio unayopitia usimsahau Mungu wako.

Unapofikia mahali na kuanza kuona wewe ndio kila kitu na ukafikiri umefika hapo ulipofika mwenyewe ni hatari sana. Kwa vyote ulivyonavyo wa kusifiwa ni Mungu peke yake badala ya kujisifu kwa uwezo mkubwa ulionao au mafanikio uliyoyapata mshukuru Mungu. Sifa ndio zinazowapoteza wengi wanapofikia mafanikio makubwa hasa vijana. Katika dunia ya sasa unyenyekevu ni wa muhimu sana ili tuweze kudumu kwenye mafanikio.

Hasa vijana hili la starehe limewakumba wengi sana  na kuwafanya kupoteza kila walichokua nacho zikiwepo pesa, umaarufu na hata sifa njema kwenye jamii. Vijana wengi wakipata mafanikio au umaarufu wanawehuka na kusahau kwamba safari bado. Wanaona wamefika mwisho wa safari yao. Kumbe mwisho wa safari yetu ya mafanikio ni kifo. Wanajiingiza katika starehe zisizofaa, wanatumia pesa hovyo, na mwishoe hupoteza vyote. Ipo mifano mingi unaweza kua nayo katika kipindi hiki kwa vijana waliofanikiwa sana na kufahamu kisha kujiingiza katika madawa ya kulevya, wanawake, pombe kupindukia, kujiuza, kucheza picha za uchi na kadhalika. Huu ni ukosefu wa maarifa katika vichwa vyao. Hivyo wewe kama unataka mafanikio na udumu katika hayo basi ni vyema ukachunga sana katika matendo hayo. Haijalishi unafanya kazi kwa bidi kiasi gani kama utakua unakosea vitu vidogo kama hivi mafanikio yako yote utayapoteza.

Soma: Tofauti ya Tajiri na Maskini ni Hii

Wengi pia hujisahau sana na kuanza kufanya mambo ya kawaida sana na kutokuweka ubora tena. Unaposahau kwamba kilichokufikisha hapo ni ulipofanya kazi kwa bidi na ubunifu wako zaid ukaanza kufanya mambo ya kawaida basi utakua unapotea taratibu na mwishoe ukasahaulika kabisa. Ukijisahau watu wanakusahau. Wateja wako wanakusahau. Kitu cha kufanya ni kuongeza ubora kila siku ili uendelee kupanda viwango.

Kuwadharau wengine ni jambo ambalo nimeliona sana kwa watu wanaopata mafanikio au kuapata cheo kikubwa Zaidi. Usifanye makossa haya kama unataka mafanikio yako yadumu. Tambua kwamba kila mmoja anamhitaji mwenzake. Hakuna aliefikia pale alipo mwenyewe hivyo usimdharau mwingine kwa kua wewe upo juu kuliko yeye. Ipo siku na yeye ataweza kufikia mafanikio makubwa sana kuliko wewe. Hata kama unaimba vizuri sana utahitaji watu wa kusikiliza nyimbo zako maskini na matajiri, hata kama una pesa sana utahitaji watu katika kuendeleza vitu vinavyokuingizia pesa. Hata kama wewe umeshakua kiongozi mkuu sana wa nchi bado upo hai unahitaji wengine katika shughuli mbalimbali za maisha yako. Angalia hao unawadharau bila wao ungefikaje hapo ulipo. Bila watu hapo ulipo sasa ungefika mwenyewe?

Wengi wanasahau kwamba mafanikio sio hatma na hivyo wanapofikia hatua Fulani hufikiri ndio mwisho wa mafanikio. Chochote unachokifanya sasa hivi mtu mwingine anaweza kukifanya pia. Hivyo kama wewe utafanikiwa kwa kiasi Fulani kisha ukaona ndio mwisho wa kufanya wenzako watakuja na watafanya kwa ubora Zaidi yako na utaondoka katika historia. Haijalishi umefikia kiwango gani ukijisahahau unaweza kupotea kabisa. Kitu cha muhimu cha kutambua ni kwamba mapambano ni hadi mwisho wako wa kuwepo hapa duniani usikubali kupumzika. Siku ukifa utalala sana na wala hakuna atakaekusumbua sumbua tena.

Ukiona umefika hatua ambayo hutaki kujifunza kwa wengine au kwenye vitu vinavyokuzunguka ujue unaanza kupotea. Ukiona umefikia hatua ambayo hushauriki unawaona wanaokushauri hawajui fahamu ya kwamba unakaribia kuanguka. Ukiona unapiokosolewa hutaki kusikia wala kujiangalia ni wapi unapokosea fahamu tu kwamba umeshalewa mafanikio na siku si nyingi utapotea. Hivyo kitu cha muhimu sana ni kubadili mtazamo wako na kuanza kujifunza kila siku kwenye kila kinachokuzunguka.

Mambo haya yapo katika maisha yetu ya kila siku jambo la muhimu sana sio kuacha kufikia mafanikio makubwa kwa kuogopa kupoteza bali ni wewe kujua ni nini kitakufanya upoteza na ukirebishe. Naamini kwa kupitia haya ukiyaweka kwenye vitendo utadumu katika mafanikio.

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading