Habari rafiki na msomaji wa blogu hii. Jumapili yako imekwendaje? Leo tunakutana tena katika kona hii ya kujifunza. Nimekuandalia mambo 20 ambayo unapaswa kuyafahamu wewe kijana. Jifunze na uyafanyie kazi. Usisahau kujiunga na blog hii ili uendelee kujifuza Zaidi.

  1. Kwanza tambua kwamba miaka 15 ijayo utakuwa na watoto ambao watakuwa wanakulaumu na kukulalamikia kwa hatua ambazo hukuchukua kwa umri wako sasa hivi.
  2. Fahamu kwamba upo kwenye umri wa kuyaandaa maisha ya familia yako uwe wa kike au wa kiume una jukumu la kuandaa aina ya maisha unayotaka kuja kuishi wewe na familia yako.
  3. Fahamu ya kwamba una majibu unatakiwa uje kuwapa watoto wako, majibu ya maana ya maisha uliyoishi.
  4. Fahamu kwamba wewe ndie unaweza kuwatengenezea watoto wako mwanzo mzuri wa kutimiza ndoto zao hivyo ukizembea sasa hivi ujue utawapa shida wanao.
  5. Muda ulionao sasa ni wa kutengeneza timu ya kukusapoti kwenye ile ndoto yako kubwa au kipaji chako hivyo kaa vizuri na kila mtu achana na kujenga chuki na watu. Wapende watu waheshimu watu.
  6. Fahamu kwamba chochote unachoamua sasa hivi kinakuja kuleta matokeo gani miaka ya mbele usiende kichwa kichwa tu. Mwanaume/mwanamke unaekubali kuwa nae sasa hivi unamwona wapi miaka mitano ijayo? Usikubali kuingia tu kwenye mahusiano hovyo hovyo.
  7. Jifunze kujiheshimu mwili wako haumstahili kila mtu, ukiwa wa hivyo unaishusha thamani yako. Hakuna ambaye anaweza kufanya maamuzi ya maisha na wewe kama huwezi kujiheshimu. Kuvua nguo zako kwa kila mtu ni kutokujiheshimu.
  8. Fahamu kwamba miaka kumi na tano ijayo kuna hadithi unatakiwa uje uitoe kwa watoto wako. Kama wazazi wako walishindwa kuwa mfano wa kuuiga wewe usikubali wanao washindwe kuja kujifunza kwenye maisha ya ujana wako.
  9. Huu ndio muda wa kuchagua jambo moja ambalo utambana hadi lije kutambulisha jina lako, ni muhimu sana ukafikia hatua ya kuwa na jambo unalofanya na utalifanya hadi siku unaondoka hapa duniani.
  10. Usiogope kukosea lakini nazungumzia kukosea unapojaribu vitu vipya vinavyoleta matokeo chanya kwenye maisha yako.
  11. Usikubali kuwa mfuasi tu jifunze kuwa kiongozi wewe mwanaume kuna watoto wako wa kiume watakuja kujifunza kwako na utakuwa kiongozi wao. Wewe mwanamke kuna mabinti utakuja kuwazaa na utakuwa kiongozi wao hivyo jifunze kuwa kiongozi.
  12. Sio kila mtu anakufaa, sio kila rafiki anafaa kuambatana nae. Angalia vyema unaowachagua wanaweza kuwa sababu ya wewe kuangamia au kufikia mafanikio. Dunia imejaa watu waovu na wasioelewa hata wakieleweshwa hata hiki nilichoandika sio kila mtu ataelewa.
  13. Tengeneza picha ya maisha yako unayotaka kuja kuishi miaka kumi ijayo uanze kuifanyia kazi. Fanya chochote sahihi hadi picha yako ianze kupata mwelekeo.
  14. Usichagua ndoto ndogo unajiwekea ukomo wa uwezo wako. Chagua ndoto kubwa na uzifanyie kazi. Ondoa hofu ndani yako ona kuwezekana kwa kila unalofanya. Una uwezo mkubwa sana ndani yako kadiri unavyoendelea kuutumia ndio utagundua ukubwa wake.
  15. Endelea kufanya kila siku bila ya kukata tamaa kile ulichochagua kufanya. Watu bado wanahitaji kukusikia usikatishwe tamaa na mtu ambaye hajakubali unachofanya. Unajua unapotengeneza kiatu namba 40 ni kwa ajili ya mtu mwenye mguu huo. Sasa kama aliekuja kujaribu ana mguu mkubwa Zaidi au mdogo asikukatishe tamaa ya wewe kuendelea kutengeneza viatu mteja wako sahihi atakuja. Hivyo pia kwenye unachokifanya usikatishwe tamaa na mtu ambaye hajakubali kazi yako.
  16. Chochote kila unachokianza sio lazima uwe umekielewa vizuri kabisa wewe endelea mbele utaanza kuona mwangaza na picha kubwa Zaidi kadiri unavyofanya.
  17. Usikubali maoni ya watu yakapoteza mwelekeo wako. Kila mtu kuna namna anavyoona sasa mwono wako usiyumbishwe na miono ya wengine jifunze kusimamia kitu kimoja hadi kilete matunda.
  18. Fahamu kwamba watu wengi wanaomiliki vitu vikubwa sasa hivi walianza kama wewe. Jifunze kwao usipende makuu kabla hujawa mkuu. Endelea kujishusha unachokifanya kitakuinua hadi sehemu usiotarajia.
  19. Tengeneza mahusiano bora kwani ukikosea hapa miaka kumi ijayo utakuwa ni mtu wa kujuta. Anza kuwa yule mtu unaetaka kuja kuwa nae. Ukitaka mwenye tabia njema anza kuwa na tabia njema wewe. Ukitaka anejiheshimu anza kujiheshimu wewe. Ukiona unakutana na watu wabovu anza kujitazama wewe mwenyewe utakuwa una matatizo ndani yako. Labda unaenda kwa hisia hutumii akilia au ndio tabia zako mbovu.
  20. Kocha wangu Amani Makirita anasema hoji kila unachoambiwa au kusikia usikubali tu kwasababu sio kila unachosikia na kuona ni uhalisia, unapohoji na kuuliza maswali unajipa nafasi ya kufahamu Zaidi na Zaidi.

Inawezakana hadi sasa kuna jambo unafanya na hujaona matunda yake. Kuna mengi unapaswa kujifunza ili uweze kuvuka hapo ulipo. Jiunge na USIISHIE NJIANI ili ujifunze mbinu mbalimbali za kukuwezesha kufikia ndoto zako.

Asante sana rafiki yangu kwa kusoma Makala hii jifunze karibu sana kwenye blogu hii tuendelee kujifunza Zaidi.

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading