Mambo 5 Ambayo kila Mjasiriamali Anapaswa Kuwa Nayo.

By | February 20, 2018

Habari za leo ndugu msomaji wa makala hizi kila siku ndani ya USIISHIE NJIANI. Ni matumaini yangu unaendelea vyema na maisha yako.  Leo tunazungumzia mambo ambayo kila mjasiriamali anapaswa kua nayo ili aweze kufanikisha kile anachokifanya. Tujifunze pamoja.

1. Mbunifu

Mjasiriamali yeyote kama unataka kua wa tofauti na wenzako na kuleta thamani kwa mteja wako unapaswa kua mbunifu.

Jaribu kuifahamu vyema biashara yako ili uweze kubuni njia mbali mbali za kuikuza.

Fahamu ni nini hasa mteja anataka kutoka kwako na ujue jinsi ya kumpatia kwa ubora wa hali ya juu ili asiweze kwenda kwa mwingine.

Sasa hivi tupo kwenye Information Age. Kizazi cha taarifa kila kitu siku hizi ni mtandao jaribu kubuni njia za kuwafikia wateja wako sehemu walipo kwa urahisi zaidi.

Kua mbunifu kwenye namna unavyotangaza biashara yako siku hizi mambo yamekua ni rahisi sana.

2. Mvumilivu

Mjasiriamali yeyote ambaye hana uvumilivu huwezi kumuita ni mjasiriamali. Lazima utambue kwamba umeingia katika sekta ambayo utapitia mambo magumu ya aina mbali mbali. Kwenye ujasiriamali unakwenda kujenga biashara yako kubwa mwenyewe hivyo wakati mwingine wengine hawatajua unachokipigania wata kuacha mwenyewe Inawezekana ni mke wako au hata mume, ndugu jamaa na marafiki wanaweza kukukimbia vumilia maana wao hawajui kile unachokipigania,  hawajui kile unachotaka kujijenga.

Inawezekana umeanzisha biashara ikafa bado haimaanishi ujasiriamali umeisha vumilia na anza tena.

Uvumilivu utaletwa zaidi na kile unachokitaka kwenye maisha yako. Ni ndoto gani uliyonayo unataka kuitimiza kwa kupitia unachokifanya?  Hiyo ndoto ndio ikufanye wewe uweze kua na Uvumilivu hata wakati ule umeanguka. Umekataliwa au umeachwa.

3. Mthubutu

Mjasiriamali lazima uwe mthubutu. Usiogope kuchukua hatua kama kuna kitu Umeona kinaweza kukuza kubadili biashara yako kifanye bila kuogopa. Kama umepata wazo jipya lifanye bila kuogopa.  Usiogope watu watasema nini juu yako. Maana hata wakisema bado wewe ndio una shida zako na unatakiwa uweze kuzitatua. Thubutu kwenda mbele hatua nyingine zaidi. Thubutu kufanya mabadiliko kwenye biashara yako.

Thubutu kua mbunifu.

4. Anaejifunza kupitia changamoto.

Kama umechagua kua Mjasiriamali unatakiwa utambue kwamba changamoto ni kitu ambacho huwezi kukikwepa. Huwezi kukwepa changamoto.

Changamoto ndio zinakufanya wewe ukomae.

Changamoto zinakujengea msingi mzuri wa biashara yako na wewe binafsi.

Ili uweze kuja kua mtu mkuu hapo baadae lazima ukubali kupitia changamoto nyingi.

Usiwaone matajiri wakubwa kama kina Mengi, Bakhresa na wengineo wamesimama kwenye utajiri wao muda mrefu bila kuyumba ukafikiri ni uchawi. Walikopitia ndio pamewajengea msingi imara na hata sasa unawaona wamesimama. Chukulia changamoto kama ni shule yako jifunze na mwisho wako utakua mzuri.  Unapopitia changamoto usilalamike wa kulaumu.

Kesho yako inakwenda kua bora.

5. Mwenye Maono.

Mjasiriamali lazima uwe na maono. Maono ninayozungumzia mimi ni makubwa. Hapo kwenye ukubwa tunatofautiana vipimo sasa wewe pima mwenyewe kisha uyatambue vyema maono yako. Kwa kifupi ni kwamba kwenye biashara yako unataka uifikishe wapi? Miaka kumi au ishirini ijayo unataka mtaji wako ufikie kiasi gani?  Miaka kumi ijayo unataka biashara yako ienee hadi wapi? Miaka mitano ijayo unataka uajiri wafanyakazi wangapi? Hivyo ni vitu vya msingi unatakiwa uwe navyo kama mjasiriamali. Maono ni kitu cha muhimu maana yanakupa mwelekeo wa biashara yako na mwelekeo wako binafsi huwezi kuyumbishwa na vitu vinavyotokea kama una maono.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *