Habari Rafiki unaendeleaje na safari ya mafanikio? Maisha ni kupambana, katika zama zote wanadamu wenzetu wamekuwa wanafanya kazi na kupata matokeo ya kazi. Kila unachokifanyia kazi kama kuna watu wanakiona ipo siku kitaleta matokeo hivyo usiogope.

Biashara ni Mahusiano.

Kama wewe una biashara na huna mahusiano mazuri na wateja wako inakuwa ni ngumu sana mteja kurudi kwako mara ya pili. Kama mteja akiwa dukani kwako hajaweza kutabasamu hata mara moja una hatari kubwa sana. Sio kila mmoja atapenda kufanyiwa kitu hadi atabasamu lakini hakikisha unafanya vitu ambavyo mteja akiondoka anapakumbuka kwenye biashara yako.

Baishara ambayo unafanya na mteja ambaye hafiki kuchagua bidhaa wewe unamchagulia inahitaji uwe na mahusiano mazuri sana. Hii ni kwasababu kwa mara ya kwanza ukianza kumpatia mteja kitu ambacho hakuagiza atarudi alipokuwa anahudumiwa mwanzo. Asiporudi basi atauliza marafiki zake sehemu bora Zaidi ya hapo kwako.

Jenga mahusiano kwa hudumua bora na bidhaa bora kwa wateja wako.

Unaweza Kuanza Popote

Haijalishi huna nini hapo ulipo bado una nafasi ya kuanza kile unachokitaka. Tatizo ni pale unaposhindwa kuona fursa zilizokuzunguka. Na unashindwa kuona fursa kwasababu unazitazama kwa macho ya kushindwa. Unatazama kwa macho ya kukata tamaa. Unataka kumiliki kiwanda sio lazima uanze moja kwa moja na kiwanda kikubwa, anza na viwanda vidogo vidogo vikuze hata ufikie kiwanda kikubwa.

Kuna mambo usipoyabadilisha yatakubadilisha wewe. Anza na nafasi uliyonayo. Ili fursa nyingine zionekane ni hadi pale utakapoanza na fursa ndogo ndogo zilizokuzunguka.

Unaweza Kujifunza Ujuzu Wowote.

Kitu chochote ambacho wengine wanafanya na wamejifunza hata wewe unaweza kujifunza na ukafanya. Bahati nzuri sana kipindi hiki sio lazima uende darasani, kwanza ujuzi mwingi wa kufanyia kazi huku mtaani haufundishwi shuleni. Unaweza kujifunza kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kujifunza kwa kuwatafuta wanaofanya ukaona na ukafanya.

Ukiishia kulalamika na kutoa sababu, eti huju hiki, hujui hiki, utabaki hapo ulipo na hakuna mabadiliko utakayoyaona.

Ukosefu wako wa Taarifa Ndio mtaji wa Wenzako.

Kile usichokijua ndio unawalipa wanaojua. Kama kuna jambo lolote ambalo hulijui na linakufanya utoe pesa kila siku kwa ajili yako embu jifunze. Ukifahamu utaacha kutoa pesa na wakati mwingine utafanya mwenyewe.

Ni kweli sio kila jambo utaweza kulifanya mwenyewe lakini kuna mambo ya msingi ukiyajua unapunguza pesa ambazo ungezitumia kwenye mambo mengine. Na wakati mwingine unaweza kuwafanyia wengine wakakulipa pia.

Changamoto yeyote unayoipitia inasababishwa na maarifa ambayo umeyakosa. Ukiyapata maarifa ya changamoto yako unakuwa umetatua changamoto na kamwe huwezi kurudi kwenye changamoto hiyo tena.

Sababu Hazikutoi Ulipo.

Sababu zozote unazotoa kwa ajili ya maisha yako haziwezi kuleta mabadiliko yeyote kwenye maisha yako. Anza sasa hivi kutafuta namna ya kutoka ulipokwama na uachane na sababu.

Kama huna mtaji suluhisho sio kusema huna mtaji bali ni kufanya namna uupate huo mtaji. Anza sasa kuwaza namna ya kutatua na sio namna ya kujitetea. Hakuna atakae kuhurumia bali utaonekana mzembe.

Ukisema huna mtaji onyesha na ulichokifanya ili kupata mtaji, usiishie sina mtaji halafu? Onyesha ulichokifanya, onyesha ulichojaribu.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading