Habari rafiki,  unaendeleaje.  Leo tena tunakutana na mambo haya matano niliyojifunza siku ya Leo. Karibu sana rafiki yangu tujifunze pamoja.

1. Uaminifu ndio Mtaji Wako.

Hakuna binadamu mwingine atakaependa kufanya kitu chochote na wewe kama huna uaminifu.  Hakuna atakaependa kuwa na wewe kwenye mahusiano. Hakuna atakaependa kufanya biashara na wewe. Hakuna atakaependa kukupa kazi.

Kabla hujaingia kwenye biashara au jambo lolote linalohisisha binadamu wenzako anza na uaminifu.

Uaminifu ni kutekeleza yale unayoaihidi, kusimama imara kwenye kile unachoamini bila kuyumbishwa.  Kutokusema uongo ili upate kitu fulani au uonekane mwema.

Kuwa mwaminifu kwenye mambo yote ndugu yangu.

2. Bidii Yako Ndio Itaamua Uende wapi.

Fanya kazi kwa bidii,  kuwa na uaminifu peke yake haitoshi lazima uende hatua nyingine ya kufanya kazi kwa bidii. Hii itaongeza sifa yako ambayo itaaamua watu wapende kufanya kazi na wewe.

“Huyu mtu ni mwaminifu na mchapakazi.” Bidii yako itafungua milango ya fursa mbele yako.  Katika kufanya kazi ndio utakutana na watu ambao watakupa mawazo ya maendeleo.

Kumbuka usiingie kwenye kufanya kwa bidii kama huna uaminifu utadondoka njiani hutafika popote.

3. Tatizo lolote Unaloliacha Unalifanya Liwe kubwa zaidi.

Tatizo unalopitia kama hutalitafutia ufumbuzi linaongezeka ukubwa. Kama tatizo ni kwenye mahusiano yako na unalifumbia macho au unajifanya kama hakuna tatizo ujue ipo siku litakuwa baya zaidi. Hii ni kwasababu mmoja wapo akichoka atakwenda kutafuta suluhisho kwingine.

Tatua matatizo au changamoto unazokutana nazo ukiziacha zitazidi kuwa kubwa. Ongeza uwezo wako wa kuelewa na kutatua matatizo makubwa zaidi.

4. Kadiri Unavyokua Ndio Changamoto zinaongezeka.

Kama jana ulikuwa hatua fulani ya maisha ukafanikiwa kusogea mbele, unakuwa umekaribisha changamoto nyingine zaidi. Unapongezeka unaongeza matatizo.

Mfano wewe una biashara yako,  imekua kiasi ulikuwa mwenyewe sasa hivi umeajiri watu watano. Hapo ujue umeongeza changamoto kwenye biashara maana kila mtu anakuja na tabia zake,  mwingine atakuwa mvivu, mwingine sio mwaminifu. Hivyo akili yako itafanya kazi zaidi kwenye kuwaangalia watu ulioajiri na bado biashara Imekuwa kubwa zaidi.

Umeoa mmeongezeka matatizo nayo yanaongezeka kama wewe ulikuwa na tabia zako fulani fulani hivi ujue na mwenzako atakua nazo.

Kila hatua unayosogea ina changamoto zaidi. Lakini ni vibaya sana kubakia sehemu ile uliyopo kwani ni matatizo zaidi ya unavyofikiri.

5. Kitu gani Mtu akikigusa kwako anagusa maisha yako?

Kila mmmoja ana sehemu ambayo hataki mtu alete mchezo kabisa. Sehemu ambayo ukikuta mtu anafanyia mzaha basi unaweza kugombana nae hata kama hujui kugombana.

Inawezekana ndio kitu ulichokipigania muda mrefu hadi kikasimama. Inawezekana ni mtu unayempenda sana.

Kila binadamu ana kitu ambacho hayupo tayari kuona mtu anakifanyia mzaha au kukipoteza.

Wewe umeshafahamu ni kitu gani?  Hakikisha unakifahamu mapema.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading