MAMBO 5 YA MUHIMU ILI UWEZE KUFIKIA NDOTO ZAKO.

jacobmushi
By jacobmushi
4 Min Read
Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na kupambana katika kutimiza ndoto zako. Leo ninakwenda kukupa njia mambo ya muhimu sana ili wewe uweze kuzifikia ndoto zako na maono yako.
 
Jua kusudi lako
Tunajua kabisa ili uweze kuishi maisha yenye furaha na utimilifu kwanza ni kulijua kusudi lako. Unapolijua kusudi lako la kuzaliwa hapa duniani unakua na nafasi kubwa sana ya kulitimiza na kufikia malengo na ndoto zako. Kama bado hadi sasa hujajua kwanini umezaliwa tafadhali wasiliana name tuzungumze nikuonyeshe namna ya kujua kusudi lako. Siku zote mtu aliepotea ahitaji kuhamaishwa anahitaji kuonyeshwa njia sahihi na namna ya kuanza upya. Ukimhamasisha anazidi kupotea. Hivyo ni muhimu sana kufahamu kwanini umezaliwa duniani. Huu ndio msingi wa mambo yote tuyafanyayo duniani.
 
Kua na Andika chini maono, ndoto, malengo na mipango
Ukitambua kwanini upo duniani haitoshi inakua sawa na nyumba ambayo imejengwa msingi peke yake. Hiyo hatuwezi kusema ni nyumba kamili lazima na ukuta ujengwe hadi nyumba ikamilike. Kwenye kuliishi kusudi lako unatakiwa uwe na maono. Maono ni ile picha kubwa ya kusudi lako yaani kule unakotaka kufikia. Ndoto na maono havitofautiani sana ila ndoto tunaweza kuweka kwenye upande wa vitu ni vitu gani unataka kua navyo viorodheshe vyote  na andika chini ni baada ya muda gani unataka kua na vitu hivyo. Weka malengo ya muda mfupi na muda mrefu. Malengo yanagwanya vipande vipande ile picha yako kubwa unaanza na vitu vidogo vidogo vya muhimu hadi ufikie vikubwa. Tengeneza mpango wa kutimiza maono yako na ndoto zako. Fanyia kazi mpango wako hadi uone matokeo kila siku.
Jua ni watu gani unawahitaji
Ili uweze kuendelea kusonga mbele hakikisha unawafahamu watu unaowahitji kwenye kutimiza ndoto zako. Kuna watu wa kukuongoza, watu wa kujichanganya nao, watu ambao utakwenda kuwagusa. Ukiwafahamu hawa watu huwezi kupoteza muda na watu usiowahitaji kwenye kutimiza ndoto zako. Jichagulie marafiki ambao wana maono na ndoto kubwa kama zako, jichagulie watu ambao watakushauri wewe kufika kule unakotaka, jua ni watu wa aina gani unakwenda kuwagusa na hilo kusudi lako. Mfano wewe ni Daktari ulizaliwa ili uwe Daktari, watu unaokwenda kuwagusa ni wagonjwa pamoja na watu wanaotaka kuweka afya zao salama. Ukiweza kutambua watu unaowagusa utafahamu kwa kuanzia. Unaweza kupanga unawezje kuanza kuwagusa watu hao kwa njia ambayo haihitaji gharama kubwa sana na watu hao maisha yao yakawa bora.
 
Kua na nidhamu
Jijengee tabia njema ambazo zitakufikisha kule unakotaka kufika. Jua ni tabia gani hazifai kabisa kwenda nazo na uziache. Kua na nidhamu ya fedha, acha kudharau wengine hata kama hawajui, hawajasoma, maskini, acha kabisa usidharau mtu yeyote. Nidhamu katika kufanya na kutekeleza kile unachokiahidi kwa watu. Yako mambo mengi sana hapa kwenye nidhamu ya kuyafanyia kazi.
 
Fanya kila siku mpaka uone matokeo.
Fanya kila siku hakikisha unaanza kidogo kidogo hata kama unasema huna mtaji au huna pesa tafuta ni namna gani unaweza kuanza kufanya bila pesa kubwa na kidogo kidogo utajikuta umefikia hatua kubwa sana. Acha kulalamika tafuta suluhisho la matatizo unayopitia. La sivyo utashindwa kuendelea mbele.
Asante sana kwa kufuatana name ukiweza kuyafanyia kazi mabo hayo hapo kuna hatua kubwa sana utakua umepiga.
Jacob Mushi,
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading