Habari za leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Natumaini leo yako inaendelea vyema. Tunakwenda kuangalia mambo matano yanayoonyesha kua unachokifanya sio kusudi la wewe kuwepo duniani. Karibu ujifunze pamoja name.

Kukosa furaha.

Kama unachokifanya hakikufanyi unakajisikia furaha ndani ya moyo wako yaani hufurahii kukifanya moja kwa moja hilo sio kusudi lako. Kaa chini tafakari ujue ni kitu gani kinafanya moyo wako uwe na furaha Zaidi. Tuseme labda umeajiriwa unakwenda kazini kila siku lakini hufurahii kazi yako. Ukiwa kazini unawaza Zaidi muda wa kufunga. Ukiwa nyumbani ukiifikiria kesho unatamani ingekua ni siku kuu. Hiyo ni shida tayari jaribu kuangalia ni kitu gani ukikifanya kinaleta furaha kutoka ndani. Kama utafanya jambo na huna furaha ndani yako huwezi kuleta matokeo bora hata siku moja ni bora tu ukaacha. Furaha yako yote inatakiwa iletwe na wewe kugundua na kuanza kuishi kusudi lako.

Kukosa hamasa

Kama unafanya jambo na halikuhamasishi mara zote unakua chini huna Amani wala huoni mwisho wako mzuri wa hicho ukifanyacho mara nyingi hakiwezi kua kusudi lako. Kusudi lako ukilifanya lazima ufurahie. Tuseme wewe ni mwimbaji halafu unapanda jukwaani huimbi kwa hamasa hata mashabiki zako hawawezi kuhamasika kukusikiliza. Kile unachokifanya kinatakiwa kianze kukuhamasisha wewe mwenyewe kwanza. Mfano mwingine ni mimi ninavyoandika ninaandika kwa hamasa na furaha maana ni kitu kinatoka ndani yangu sichoki wala sikati tamaa. Hata nikipitia changamoto hazinirudishi nyuma na wakati mwingine kwa kupitia hizo changamoto ninapata vitu vya kuandika. Hivyo ni muhimu na wewe ujitafakari kwa kina kama ukifanyacho kinakupa hamasa kama hapana nab ado huna furaha ukifanyapo basi chukua hatua ukajitafute ugundue wewe uko bora upande upi.

Kushindwa mara nyingi.

Kama unachokifanya unashindwa kila wakati yaani wewe kila unapofanya hua unashindwa tu. Hujawahi kusogea mbele hata mara moja basi maana yake wewe unachokifanya sio kusudi lako. Kama si hivyo basi ni kwamba unafanya sehemu ambazo hauko bora Zaidi. Nikiwa na maana kwamba kama unafanya jambo lakini unashindwa kila siku halafu jambo hilo ndio linaupa furaha moyo wako na unahamasika nalo inawezekana hujifunzi au unafanya kwenye ile sehemu ambayo wewe ni dhaifu. Ni sawa na mwimbaji wa Reggae ajaribu kuimba R&B hatafanya vizuri na mar azote ataonekana kushindwa. Inawezekana unashindwa jambo sio kwasababu sio kusudi lako ila ni kwakua unakosea unapambana sehemu ambayo wewe ni dhaifu. Wanafunzi shuleni mara nyingi unakuta kuna ambaye somo la Hesabu ni bora Zaidi kuliko masomo mengine wengine unakuta somo la Kiswahili ndio bora kwake. Sasa wa hesabu akitumia muda mwingi kupambana awe bora kwenye Kiswahili atajikuta anafeli Hesabu pia alie bora kwenye Kiswahili akitumia muda mwingi kufanya Hesabu atakikuta anafeli kwenye masomo yote.

Kukata tamaa haraka.

Kama unafanya jambo na unakata tamaa unakosa kabisa hamu ya kulifanya ujue unachokifnya hakitoki ndani yako. Kuku hawezi kukata tamaa kutaga hata siku moja ukiharibu sehemu yake ya kutagia atatafuta hata kwenye kichaka atage. Hivyo kile kilichopo ndani yako hakiwezi kuzuiwa na kitu kingine. Ukiona unakata tamaa haraka kaa chini jitafakari upya inawezekana kabisa ukifanyacho hakitoki ndani yako. Hali ya hewa haiwezi kukuzuia, watu hawawezi kukuzuia, mazingira hayawezi kukuzuia ni wewe mwenyewe ndio unaamua kukata tamaa na kurudi nyuma. Hamasa iliyoko ndani yako inatakiwa ikuzwe sana na utaikuza kwa kujichanganya Zaidi na watu wanaofanya vitu kama unavyofanya au wanaotamani kufika mbali na wenye ndoto kubwa.

Kutamani kufanya jambo Jingine.

Kama kuna kitu kingine unatamani kukifanya zaidi ya kile unachokifanya sasa hivi jibu ni kwamba hauishi ndoto yako na wala hujaliishi kusudi lako bado. Yaani kama wewe unafanya jambo halafu mawazo yako yapo sehemu nyingine ni wazi kwamba hilo unalolifanya sio kusudi lako. Ni sawa na mimi nipo naandika hapa halafu moyoni mwangu niwe natamani kwenda kuimba. Nikijiangalia baadae najiona nimesimama jukwaani naimba. Hiyo inaashiria kwamba nikifanyacho hakinipi picha ya maisha yangu ya baadae. Ni muhimu sana kujua kile unachokita na ukubali kutokukiacha kamwe.

Mambo yote hayo matano ukiyatafakari na ukaona kwamba yanaendana katika kile unachokifanya ujue kabisa ukifanyacho sio kusudi lako amua sasa kuchukua hatua ya kuligundua kusudi lako.

Karibu sana. Ni furaha yangu kuona unaliishi kusudi lako maana ndio msingi wa mambo yote mazuri duniani.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

2 Responses

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading