Kinachokufanya uendelee kubaki hapo ulipo ni kwasababu unataka kufanya kile ambacho kila mtu anafanya na atakikubali. Unajua hata ukileta bidhaa yako sokoni ikakubaliwa na kila mtu hiyo bidhaa inashuka thamani haraka.

Unatakiwa ukubali kuwa wa pekee hataka kama watu watakuchukia basi iwe hivyo kwasababu wewe sio kila mtu. Kuna neon moja linatajwa sana kwenye maelezo hasa ya kushindwa au kufeli utasikia wanaseme “watu wengi” wamefanya hivi au wako vile au wanapenda hiki, sasa embu jiulize wewe ni watu wengi? Hivi unajua mmiliki wa simu ambayo inatumiwa na watu wachache duniani ndio Tajiri kuliko mmiliki wa simu ile ambayo watu wengi wanaweza kuinunua na wanaitumia tayari?

Sasa wewe Rafiki yangu usipende kuwa mmoja wa watu wengi embu kuwa kati ya wachache walioamua kujitofautisha. Yapo mambo ambayo watu wengi wanapenda kuyafanya na nimekuandikia leo ili ujitazame upo kwenye kundi hili la watu wengi au la wachache.

Kufuatilia Maisha ya watu maarufu.

Kuna watu ambao wanataka kujua kila kitu kuhusu watu maarufu na ukikaa nao utashangaa wanaweza kukueleza kila kitu kuhusu mtu huyo. Labda utaelezwa hadi idadi ya wapenzi wake wote ambao ameshakuwa nao. Utakuta mtu anafuatilia nguo au kiatu ambacho mtu maarufu amevaa na endapo atarudia nguo ile au kile kiatu basi itakuwa ni Habari wataambiana.

Ni kweli sio jambo la maana kabisa kwasababu yapo mengi ambayo ungeweza kujifunza kwa mtu na wewe ukafanikiwa kwenye kile unachokifanya. Kitu ningependa kukwambia ni kwamba watu hao unaowafuatilia Maisha yao wao hawana muda huo. Wao wako bize kufanya vitu vitokeee. Hivi wewe ni lini watu wengi wataanza kukufuatilia siku moja? Ni ile siku utaacha kufuatilia Maisha binafsi ya watu ambao hata hawakujui. Vipo vitu vingi vya maana kufuatilia kwenye Maisha ya hawa watu na vina manufaa lakini sio hivi ambavyo watu wengi wanafanya.

Watu wasio na vipaumbele ndio hupata muda wa kuafuatilia Maisha ya watu maarufu kwasababu Maisha yao binafsi sio vipaumbele vyao.

Kutumia muda mwingi kuangalia Tv na Kusoma magazeti.

Ni kweli Tv na Magazeti yapo ili yasomwe na ziangaliwe, lakini haina maana basi wewe ndio uwe mfuatiliaji wa kila kitu ambacho kinaendelea. Sio kila kitu kinatakiwa kifuatiliwe na wewe ambacho kinaoneshwa au kuandikwa kwenye magazeti na tv.

Maskini peke yao ndio wana muda wa kufuatilia kila kitu kinachoendelea. Na wana muda kwasababu hawajui nini wafanye, hawana malengo makubwa yanayowaweka bize kiasi cha kukosa muda wa kufuatilia kila kitu.

Wanatumia muda mwingi kwenye mambo yasiyowasaidia chochote.

Unajua wewe utakuwa hujaelewa hili, kama kuna kuna ambalo linachukua muda wako mwingi na halikuongezei faida yeyote kwenye Maisha basi linakuletea umaskini. Endapo tu utalipa muda mwingi sana lazima likuletee umaskini.

Kama wewe unafuatilia mambo ya mapenzi sana kuliko vitu vingine utakuwa na umaskini wa kukutosha kwasababu mapenzi hayaleti pesa labda uwe unajiuza. Kama utakuwa unafuatilia Habari za mpira kupata kiasi maana yake utakuwa hufanyi mambo mengine ya msingi na kinachofuata hapo ni umaskini. Kama utakuwa unakwenda sehemu kwa marafiki zako mnaongea masaa kadhaa mambo ambayo hayana maana sana basi utakuwa hujajua umuhimu wa muda wako na mwisho wa siku ni wewe kukwama kimaisha.

Wanachelewa kuamka.

Maskini peke yake ndie anawahi kulala na kuchelewa kuamka kwasababu hana jambo lolote kubwa ambalo linamhamasisha kuamka mapema ili alifanye litokee.

Matajiri wote wanaamka mapema ili waweze kufanya mambo makubwa kwenye Maisha yao. Sasa wewe unaweza kusema sasa Tajiri ana kila kitu anaamka mapema ya nini sasa? Si angelala hadi saa nne? Ndio hayo pia ni mawazo ya kimaskini kwasababu wanafikiri ukiwa Tajiri basi unakuwa na muda wa kulala sasa.

Kuamka mapema kunaifanya akili yako iweze kuwaza vizuri na hata kuamua vitu mbalimbali kwa umakini Mkubwa. Kuamka mapema ni afya kwenye mwili wako. Kuamka mapema kunakuwezesha kutimiza malengo yako ya siku.

Wanakula vyakula vibovu.

Unajua matajiri wanaishi muda mrefu kwasababu wanajali afya zao, wanakula vizuri. Ndio unaweza kusema sasa mimi ni maskini nawezaje kula vizuri? Nenda kasome upya lile somo la biolojia la shule ya msingi utaona mlo kamili ni n kitu gani. Mara Nyingi ni chakula kile kile ambacho unakula kila siku lakini wewe unakula bila mpangilio.

Hawana bajeti ya Maisha yao.

Kama hujui kiwango gani cha pesa unachotumia kila wiki au kila mwezi kwenye matumizi yako ya kila siku basi upo kwenye kundi hili la maskini. Unaweza kusema sasa Tajiri anaweka bajeti yanini wakati ana pesa Nyingi? Kinachomfanya yeye kuwa na pesa Nyingi ni kwasababu ameweza kuwa na bajeti ya matumizi inayoeleweka.

Wanakopa kwa matumizi yao ya kawaida.

Ulishawahi kukopa pesa ukaenda kulipa kodi ya Nyumba au kununua chakula kwasababu pesa huna? Basi tabia hii ni ya kimaskini. Usikubali kuendelea nayo Rafiki yangu. Ukikopa pesa yeyote hakikisha unaiweka sehemu ambayo itakuzalishia pesa Zaidi uweze kurudisha ile uliyokopa na ubaki na faida. Usiwe mtu ambaye anakopa anatumia kisha anaanza kutafuta nyingine ili arudishe  deni.

Yangu ni hayo tu Rafiki, ninaamini unakwenda Kuchukua Hatua, na utatimiza maono yako. Usikubali kuishia njiani.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading