Habari ya leo rafiki yangu na msomaji wa Makala hizi. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na safari ya mafanikio. Katika Makala yetu leo nitakwenda kukushirikisha vitu 9 vya kufanya ili uweze kua na maisha yenye furaha. Kwenye maisha zipo  chngamoto nyingi tunazozipitia na zinasababisha tuishi maisha ya wasiwasi,huzuni na woga wa kesho ukiweza kufanya haya tutakayojifunza leo maisha yako yatakua yenye furaha tele siku zote.


Kua mzalishaji, na mwenye maisha ya mwendelezo.

Tunaposema uwe mzalishaji haimaanishi uwe na kiwanda. Unatakiwa kwenye chochote unachokifanya kiwe kinaleta matokeo ya kila siku na yenye kuendelea. Hii itakufanya uwe na furaha na hamasa ya kuendelea kufanya zaidi. Maisha yako yatakua na muendelezo  unaoeleweka nah ii itakuletea furaha.


Jichanganye kwenye shughuli zinazoleta maana matokeo kila siku.

Hapa inategemea wewe unafanya shughuli gani. Kama wewe unafanya kile kitu unachokipenda hakikisha siku haipiti hujafanya chochote kinacholeta matokeo au muendelezo. Hii itakufanya uwe na furaha kwa kua ni kitu unachokipenda.

Tenga muda wa kukaa na watu unaowapenda. 

Katika maisha hata kama unatafuta kwa bidii kiasi gani hata kama upo bize kiasi gani hakikisha unapata muda wa kukaa na wale unaowapenda. Hii itakuletea furaha wewe na wengine pia wataona unawajali na kuwapenda.  Wanaweza kua ndugu wa karibu, mke, mume, watoto, marafiki na wale wote unaowapenda na kuwajali. Hii inaleta maana halisi ya maisha.

Tengeneza mfumo wa maisha wenye vitu unavyovipenda. 

Kila mtu ana aina ya maisha anayoyataka na anayoyapenda na yanamfanya awe na furaha kitu cha muhimu cha kuzingatia hapa unatakiwa uwe na uwezo wa kuweka vipaumbele ujue kipi ni cha sasa hivi na kipi ni cha baadae. Maisha hayajirudii utoto ulishapita haurudi, ujana utapita au ulishapita kwako angalia ni vitu gani vya kufanya ili kwa kipindi hicho unachoishi uweze kufurahia maisha. Sizungumzii anasa nazungumzia mambo yale yaliyo sahihi kutokana na Imani yako unayoiamini wewe. Fanya kila jambo kwa wakati wake. Kuna vitu ambavyo hukuvifanya ukiwa mtoto na hutakaa uweze kuvifanya tena, vile vile kwenye ujana na uzee pia.

Kua na malengo.

Kwenye maisha ya uzalishaji wenye mwendelezo uantakiwa uwe na malengo ambayo unayaweka kila wakati na unapofikia hatua fulani jipongeze unapojingeze unakua unajihamasiha mwenyewe na pia utajijengea furaha yako mwenyewe. Unapoweka malengo Fulani na ukaweza kuyatimiza unakua na hamasa kubwa ya kuendelea kufanya kaz kwa bidii na utakua unasonga mbele kufikia ndoto zako na mafanikio makubwa.

Kua na fikra Chanya.

Huwezi kua na furaha kama mar azote wewe una fikra hasi kila linalotokea kwako unafikiria hasi tu. Mfano umempigia mtu simu hakupokea na ukaanza kulaumu na kusema mabaya juu yake. Kama ni mke/mume au mpenzi wako ukaanza kumhisi labda anakusaliti. Ukiwa na fikra hasi maisha yako yote yatakua na huzuni hasira kila wakati maana kila kinachotokea kwako unakipelekea kwenye upande hasi. Ukiweza kujijengea tabia ya kufikiri chanya kwenye kila kinachotokea kwako utakua na maisha yenye furaha sana.

Zuia wasiwasi kwenye mambo yasiyo ya muhimu.

Kama maisha yako wakati wote yanakua ni wasiwasi juu ya kesho juu ya jambo lolote linaloweza kutokea utakua huna furaha. Kua na wasiwasi sio vibaya ila kwenye mambo yenye kueleweka na uwe na uwezo wa kutoa suluhisho juu ya wasiwasi wako. Ukiweza kuwa mtu wa namna hiyo utaweza kuondoa kuchanganyikiwa maramara na kukosa furaha. Unakuta mtu yupo anakula mawazo yake yanawza kesho itakuaje kazini. Uko na familia unamuwaza boss alivyokugombeza mchana huwezi kufurahia wala kua na maisha yenye Amani.


Jenga tabia ya kutoa kuliko kupokea.

Ukijijengea tabia ya kutoa kuliko kupokea maisha yako yatakua na furaha sana maana utakua umewasaidia watu wengi na wewe utakua unapokea zaidi. Kutoa ni kama kupanda mbegu ambayo ipo siku italeta mazao lakini unatakiwa utoe sehemu ambayo huwezi kurudishiwa. Ukijijengea tabia hii maisha yako yatakua na furaha.


Jifunze kuishi wakati uliopo.

Kama tulivyoona kwenye Makala nyingine huwezi kubadili chochote kilichotokea nyuma hivyo acha kuwaza yaliyopita fikiria ya sasa utakua na maisha yenye furaha sana.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading