Habari za Leo Rafiki yangu. Unaendelea kufanya kile ulichoamua kukifanya? Umeshatambua ni kwanini upo hai Leo? Mungu hajakuacha bahati mbaya. Sio kwasababu wewe ni mwema sana kuliko waliopoteza maisha yao. Sasa basi usichezee hata siku moja vibaya usiache siku yeyote ipite bila ya wewe kufanya jambo kwenye kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.

Nimeamua kukuandalia mambo matano ambayo nitakuwa nimejifunza kwa siku husika kuanzia siku ya leo. Mambo haya matano ninaweza kuwa nimejifunza kwenye vitabu, kwa watu ninaokutana nao, kwenye biashara nianzofanya, kwenye biashara za watu ninaowatembelea. Karibu sana ujifunze pamoja na mimi kila siku kupitia mambo haya.

  1. Mitazamo yetu Inaongoza Vitu vingi Kwenye Maisha yetu.

Jambo moja linaweza kutokea sehemu lakini watu kumi walio ona jambo hilo kila mmoja akaelewa kulingana na mtazamo wako ulivyo.  Kila mmoja atatengeneza picha yake kutokana na ufahamu wake ulivyo. Mara zote usishangae kuona jambo moja limemfanya mtu akapata hasira sana na mwingine akawa kimya. Kuna jambo linaweza kumfanya mtu akalia sana mwingine akaishia kusikitika tu.

  1.  Unashindwa kwenda Mbele kwasababu hujui unapokwenda.

Kama hujui unapokwenda kusema ukweli lolote unalolifanya ni sawa na kupoteza muda wako. Huwezi kuwa na vipimo vya mafanikio kama hujui unapokwenda. Hakikisha una picha kubwa ndani yako ambayo ndio inakuongoza kufanya yale unayoyafanya. Hii itakusaidia sana usibebwe na kila kinachokuja mbele yako.

  1.  Wewe ndio unaamua kushindwa au kushinda.

Kelele zozote za nje zinazosema huwezi hazina nguvu yeyote ya kukuzuia hadi pale utakapokubaliana na kelele hizo. Haijalishi wamesema maneno makali kiasi gani juu yako wewe ndio unaamua kuyapokea na kuingiza ndani ya moyo wako. Anza kukataa maneno ya kushindwa unayoambiwa. Kuna nyakati zinafika hutaweza kuwakimbia watu wanaokupinga watakuwa wamekuzunguka kila mahali hivyo unachotakiwa kufanya sio kukimbia bali ni kujua namna ya kupambana ili ushinde.

  1.  Hamasa peke yake Haitoshi

Kama utakuwa na hamasa unaweza kufanya jambo kubwa sana lakini kama huna usugu ndani yako utakwama utakapokutana na changamoto. Ni muhimu sana vyote hiki vikawa pamoja. Kuna mahali hamasa itatumika na kuna mahali usugu na kutokata tamaa kutatumika. Hasa pale unapo vunjwa moyo na watu mbalimbali.

  1.  Wakimbie watu wanaokunyanyasa.

Kuna watu wana tabia za kunyanyasa wenzao wakiona una kitu kikubwa ndani yako wanataka kukutumia vibaya. Ukiona mtu anakwambia bila mimi hutafika popote, usipopita kwangu nitafanya mpango ukwamishwe. Kuna watu wa namna hii hawa ni wa kukaa nao mbali sana maana wanaweza kukuharibu ukawaona wao ndio kila kitu kwenye maisha yako. ukiona mtu wa namna hii kaa nae mbali kabisa wala usiruhusu ajue mambo yakow ala mipango yako.

Mafanikio ni maamuzi, Ukiamua kubaki hivyo ulivyo ni wewe mwenyewe. Ukiamua kutafuta njia ya kutoka utatoka. Ukikaa chini ukakubali madhaifu uliyonayo hutakaa ubadilike. Amua sasa kufanikiwa. Penye nia pana njia. Ili watu wajitokeze kukubeba lazima uanze kuonyesha juhudi za kutoka hapo ulipo.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading