Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu ni matumaini yangu kua ni mzima na unaendelea na shughuli zako vyema.

Leo tunajifunza mambo matatu ya muhimu na ya lazima kua nayo ili uwe na furaha katika maisha yako nimejaribu kyatafakari sana nikagundua kua chanzo cha kutokua na furaha ni mtu kufanya mambo mawili na kuacha  limoja au kinyume chake.

1. Mahusiano yako na Mungu.
Hili ni jambo la kwanza la kuzingatia katika maisha yako ukiweza kua na mahusiano mazuri na Mungu utakua na furaha kwani imani yako itakua kila siku. Pia hutakua na hofu wala woga katika malengo yako na ahadi zake juu ya maisha yako Soma Kumbukumbu la torati 28:1-  hapa tunaona baraka za Mungu tukiyashika maagizo yake

2. Mahusiano yako na watu.

Mahusiano yako na watu yanaleta furaha katika maisha  yako kwa kua huwezi kuishi huku duniani mwenyewe Adamu mwenyewe alishindwa kuishi na wanyama. Ukitaka mafanikio na furaha weka msingi mzuri hapa hakikisha huna uadui wala chuki na mtu yeyote huku duniani. Na sio uwe na amani tu bali bali jdnga ukaribu na watu mbali mbali wanaoweza kukushauri ili uweze kutimiza ndoto zako. Nakuhakikishia mafanikio ni yako na ahadi za Mungu juu yako zitakujilia. Hapa pia ndio sehemu ya muhimu kwa wale ambao bado hawajaoa/kuolewa hapa ndipo unapotakiwa utengeneze wewe aina  maisha ya ndoa unayoyataka jenga mahusiano vizuri utakua na ndoa yenye furaha baadae kila kitu kinaandaliwa. (Jiandae kua baba/ mama mume/mke  bora). Kama umeoa/umeolewa pia ni nafasi yako ya kujenga ndoa na familia yenye furaha utayafurahia maisha.

3. Mahusiano yako na fedha.

Hapa tunazungumzia juu ya utafutaji wa pesa na mafanikio ya vitu kumiliki mali hapa ndio penye shida kubwa watu wengi hua wanawahi huku hayo mengine wanayaacha wanasema ni baadae. Kila kitu ni maandalizi ukitafuta pesa bila kua na mahusiano mazuri na Mungu. Hutakua kua na amani wala furaha. Ndio maana wengi hua wanaishia kwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapewe hirizi za kuwalinda. Ukikua katika njia hizi tatu hutakua na hofu wala mashaka (Epuka kua kinyume na Mungu) kua simamia unachokiamini. Ukiwa vizuri kwenye jambo la kwanza na la pili hili la tatu ukalikosa hutaishi kwa furaha. Lazima upangilie mambo yaendane usiegemee upande mmoja.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

3 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading