Habari mpendwa na rafiki msomaji wa makala zetu kupitia blog hii. Ni matumaini yangu kuwa unaendelea vizuri katika utendaji wako. Binafsi ninarudisha sifa na utukufu kwa aliye “chanzo” cha mafanikio yetu.
Leo ninawiwa kukuletea makala hii, “MAMBO 6 YA MSINGI ANAYOTAKIWA KUWA NAYO KIJANA ILI AKUBALIKE KATIKA JAMII”. Lakini acha nianze kwa kusema hivi, binafsi nina hofu kubwa sana kwa “taifa la kesho” ambalo asilimia kubwa ni sisi vijana maana tumekosa muelekeo, na kupoteza uthamani wetu.
Taifa linategemea vijana, familia kama familia inategemea vijana, makampuni mengi yanategemea vijana, hata kanisa nalo linategemea vijana, kwanini? Kwa sababu vijana tuna nguvu, yani ni tofauti na watu wa umri mwingne kama wazee na watoto. Hata biblia inasema hivyo. Lakini cha ajabu tumeshindwa kujitambua kuwa sisi ni akina nani na tunapaswa kufanya nini. Ole wetu vijana.
 
 
Kutokana na hali hii jamii imeshindwa kutupa kipaumbele kwa ajili ya kukosa a mambo haya 6 ambayo tutayaangalia japo kwa kifupi kutoka 1 Thimotheo 4:11-12,. Mwandishi anasema mtu yeyote asiudharau ujana wako bali uwe..
1. Kielelezo.
Kuwa kielelezo ina maana ni kuwa mfano, kitu cha kuigwa. Watu wa”copy” kutoka kwako. Sasa tumekuwa hatuna cha kuigwa katika jamii, badala yake ndo walevi “wanywa viroba” kuwa na tabia zisizo njema kama wizi, uporaji n.k.
Ukija kwny suala la uvaaji ndo hatari kabisa, dada zetu wanavaa nguo zinazonesha miili yao”transparency” vijana wa kiume nao suruali chini ya makalio,. Yani jamii inashndwa kutuelewa kabisa. Hebu tubadilike.
2. Usemi.
Kauli/usemi ndiyo inayomfanya mtu kukubalika mahali popote pale. Watu wanakutambua kwa jinsi unavyoongea tu. Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua kuwa vijana ndo wenye majibu ya “hovyo” mahali popote pale. Ukikuta binti anajibizana na mama yake huwezi amini kama anamjibu mzazi wake hvyo.
Sasa kupitia kauli zetu na jinsi tunavyo”communicate” na watu kumetufanya tukawa tunakosa fursa mbalimbali na hata kushirikishwa kwenye jambo lolote lile linalohitaji maamuzi au mchango wa kijana. Hali hii inatufanya tunakosa haki zetu za msingi.
3. Mwenendo.
Jamii inatazamia kuwa mwenendo wa kijana unatakiwa kuwa mzuri, lakini badala yake, inatuona tunaenenda ktk njia zisizofaa kama ukahaba, ulevi, wizi na kujiunga na vikundi vya uhalifu n,k, jamii inatudharau. Kumbuka nilianza kwa kusema kuwa “mtu yyte asiudharau ujana wako” lakni hapa sisi tunakuwa chanzo cha kudharaulika. Hebu tubadilishe mwenendo wetu na kuwa mzuri.
4. Upendo.
Kama kijana utakosa kuwa na upendo kwa jamii inayokuzunguka, itakuwa ni ngumu sana kupata msaada. Jamii itakutelekeza. Ukitaka jamii yako ikupende, ipende wewe kwanza. Kila mtu atatamani kuuona uwepo wako. Fursa nyingi zitakua zinakuangukia wewe maana una mahusiano mazuri na jamii yako.
5. Imani.
Hili ni jambo lingne la muhimu sana kwa maisha ya kimwili na kiroho. Ili umpendeze mungu ni lazma kuwa na imani. Biblia inasema kuwa “hauwezi kumpendeza mungu kama huna imani”. Jamii inapenda mtu anaemwamini Mungu, maan a hata yeye mwenyewe ataaminika. Siku hizi ofisi nyingi zinaogopa kuwaajiri vijana, kwa sababu hazina imani na sisi. Tunakosa mambo mengi kwa sababu hatuamiki. Tubadilike. Tukitaka kula “mema ya nchi” hebu tujiaminishe kwa jamii. Tusiwe watu wa kutiliwa mashaka kila mahali.
6. Usafi.
Hapa sizungumzii usafi wa kimwili tu. Maana mwili huu ni kama “mother body” ya roho zetu. Japo ni lazima uuweke katika hali nzuri. Hata biblia inasema itunzeni miili yenu maana ni hekalu la roho mtakatifu. Utakapoamua kuwa msafi kiroho, yaani kuacha mambo yote mabaya i.e dhambi, hata kimwili utakuwa safi pia. Mabadiliko huanzia ndani na matokeo ndio yanayoonekana kwa nje.
Naamini utakuwa umejifunza mengi, na ninategemea mabadiliko makubwa sana. Nimalizie kwa msemo huu, “CHANGES IN OUR SOCIETIES DEPENDS THE CHANGES OF YOUTHS FIRST”.
Karbu kwenye makala zinazofuata tuendelee kujifunza mengi.
Ubarikiwe.
Imeandaliwa na 
Steven I. Mshiu
0655882074O 
smshiu42@gmail.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading