Habari za Leo Msomaji wetu. Tunakwenda kuzungumzia kwa kifupi juu ya ajira na waajiriwa na jinsi ya kujitoa kwenye kongwa hili. Ni kweli tunategemeana katika maisha yetu mwenye biashara anategemea wafanyakazi ili aweze kukuza zaidi biashara yake. Lakini bado hiyo haitakiwi kuwa sababu ya wewe kutofanya kitu kingine na kubakia unategemea mshahara peke yake.

 Mabadiliko yanayokuathiri wewe mwajiriwa na Ajira yako.

Kwa Tanzania sasa hivi kupoteza kazi yako ni rahisi sana. Unaweza kwenda kazini leo ukakuta umefukuzwa. Teknolojia inabadilisha kila kitu. Baada ya muda mfupi unaweza kukuta kazi yako inafanywa mashine. Huna uhakika na kampuni unayofanya nayo kama itabaki miaka 20 mbele inaweza pia ikafa. Kumbuka Sikwambii haya kukutia hofu ni Ukweli ili ujiandae Lolote laweza kutokea.

Mambo uliyokua huyajui.

• Hakuna Tajiri alieajiriwa matajiri wote wanamiliki biashara zao wenyewe. Usifikiri kua tajiri kwa kupitia kwenye ajira.

•  Huwezi kua tajiri kwa kutegemea mshahara wako anza sasa kufikiria na kufanya, buni mfumo utakaokutengenezea kipato wakati upo kwenye ajira kipato hicho kikizidi mshahara na fanya mpango uache kazi.

•  Kama hujui ni kwamba boss wako hana mpango wa kubadili maisha yako furaha yake yeye ni aone unamfanyia kazi kwa bidii. Ukiumwa leo ukabaki nyumbani miezi mitatu ukirudi kazini utakuta nafasi yako imeshachukuliwa.

•  Haijalishi una elimu kubwa kiasi gani au ndogo kiasi gani mwajiriwa ni mwajiriwa tu wote wana hatari moja/wote wanamfanyia kazi mtu, ukifukuzwa kazi leo maisha yako lazima yatayumba.

•  Kilio kimoja cha kila mwajiriwa ni mishahara haikutani. Unaweza kubadili hali hiyo leo kwa kua na mfumo wako unakutengenezea pesa nje ya ajira.

•  Usipoteze muda kuomba uongezewe mshahara au upande cheo waza kumiliki biashara yako mwenyewe.

•  Mshahara ukiongezeka ujue utatakiwa ufanye kazi nyingi zaidi/uzalishe Zaidi, ukipanda cheo ujue na majukumu yatakua mengi Zaidi. Pesa utakayoongezewa huwezi kuifurahia tena.

•  Kwenye mfumo wako mwenyewe ni kwamba kuna wakati utakua haupo lakini pesa zinaendelea kutengenezwa.

Soma na Hii: VITU VYA KUFANYA ILI UWE NA UHURU WA KIFEDHA

•  Kama unafarijiwa na mafao utakayopata uzeeni piga mahesabu ni kiasi gani utapokea na uone jinsi gani unapoteza muda.

•  Mafao unayoyasubiria baada ya miaka 40 ya ajira ungeweze kutengeneza mara  50 yake na kwa muendelezo yaani hiyo miaka 40 ya ajira ni miaka 5 tu inaweza kukufanya wewe uanze kuishi maisha ya kipato kinacholingana na mafao yako.

•  Ajira yako haikulindi bali inakufanya uwe mtumwa unauza muda na nguvu zako kila siku kipato ambacho siku zote hakitakaa kikutoshe.

•  Sikwambii haya ili uache kazi leo lah! Anza kujitengenezea mfumo leo ili undoke hapo bila maumivu wala hofu yeyote.

•  Zipo biashara nyingi za kuanza ukiwa kwenye ajira lakini changamoto kubwa ni kwamba zitakukosa wewe kwasababu upo kwenye ajira hivyo ukuaji wake utakua kwenye hatari kubwa sana.

•  Lakini zipo biashara ambazo unaweza kutenga ule muda wako wa ziada baada ya ajira ukawa unaikuza biashara hii na ikakuletea mafanikio makubwa sana.

Inawezekana wewe hujawahi kufikiria kua tajiri au kumiliki mali nyingi biashara zako na kadhalika lakini kujiajiri au kua na kipato cha ziada ni kitu cha muhimu kwa maana unakua hutegemei mshahara peke yake.  Lolote linaweza kutokea kipindi hiki.  Kua makini na jitengezee njia za kukusaidia kabla mabaya hayajakufikia.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Jiunge na Usiishie Njiani Academy Hapa https://jacobmushi.com/academy/

Huduma Zetu https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading