Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu. Ni furaha yangu kusikia unaendelea vyema na mapambano. Leo tunajifunza mambo matatu ya muhimu unayotakiwa uyapate ndani ya mitandao ya kijamii.  Mitandao hii imekua ni sehemu ambayo wengi wetu tunapoteza muda bila kufanya chochote cha maendeleo Kwenye maisha yetu. Ni muhimu sa ujifunze namna ya kuokoa muda wako usipotee bure bila faida.

 

1 . Maarifa

Kama wewe kila siku unaingia Kwenye mitandao hii na hupati maarifa yeyote na badala yake unakutana na habari za mambo yanyoendelea duniani unapoteza muda. Hakikisha kila siku unapoingia Kwenye mitandao hii uwe na mahali unajifunza kitu iwe ni Whatsapp au Facebook lakini uongeze maarifa ndani ya akili yako.

La sivyo utajikuta umekua mtumwa na mpotezaji wa muda Kwenye mambo yasiyo na faida kwenye maisha yako. Mara nyingi Kwenye mitandao hii ukiingia utakutana na habari fulani inayojadiliwa na inavutia sana kujua ni nini kinaendelea.

Kama jambo unalolifuatilia haliongezi thamani yako, kiroho, kiakili na kiuchumi ni kupoteza muda. Kama halifanyi maisha yako yakawa bora kwa namna fulani ni kupoteza muda. Ni sawa na mtu anaekula chakula kisichokuwa na virutubisho vyovyote mwilini mwako.

Soma: Kitabu Siri 7 za Kuwa Hai Leo. 

  1. Mahusiano Bora na Wengine.

Mitandao hii itumike kutengeneza Mahusiano bora na wengine kwani kupitia mahusiano haya utaweza kufungua milango mbalimbali ya fursa na kuwezeshana.

Kupitia mitandao hii ukiweza kuitumia vyema kama una bidhaa zako unauza utatengeneza wateja.

Kama wewe unatumia mitandao hii kupeleka majungu kwa wengine au kuonyesha mambo yanayoendelea kwenye maisha yako utakua unapoteza muda tu. Kuna watu wakiachwa wataandika Facebook, wakipata wapenzi wapya wataandika tena. Sio vibaya kuweka kinachoendelea maishani mwako lakini lazima ujue kipi ni cha kuweka na kipi sio. Mara nyingi watu hupenda kuweka mambo ya furaha yanayoendelea maishani mwao. Sio vibaya hata mimi napenda kufanya hivyo lakini kwa nia njema ya kutengeneza mahusiano bora na Wengine.

  1. Pesa.

Unaweza kutengeneza pesa kwenye mitandao hii ya kijamii kwa njia mbalimbali sana. Kama nilivyosema upate maarifa,  utengeneze mahusiano bora na wengine kisha utengeneze pesa. Kama una ujuzi au kipaji chochote angalia ni kwa namna gani unaweza kutumia maarifa haya kutengeneza pesa,  mitandao hii imejaa watu wengi mno unaweza kubuni namna za kuwafikishia kile unachokifanya.

Njia zipo nyingi za kuuza bidhaa au kipaji chako kwenye mitandao hii.

Kwanza unatakiwa umiliki blog yako ambayo inaeleza kile unachokifanya.

Labda nikwambie tu mimi hapa 90% ya wateja wangu kwenye vitu ninavyofanya nawapata kwenye mitandao ya kijamii.

” Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

2 Responses

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading