MAMBO YA MUHIMU KUTAZAMA ILI TUWEZE KUONA MWANGAZA WA MAFANIKIO KILA WAKATI

jacobmushi
3 Min Read

Tangaza msamaha
Tangaza msamaha kwa waliokutendea mabaya yeyote kwenye maisha yako.
Ulitelekezwa ukiwa mtoto mdogo tangaza msamaha leo. Uliumizwa na mpenzi wako uliempenda sana hata ukasema hutakaa umsamehe tangaza msamaha leo. Ulidhulumiwa chochote na mtu mtangazie msamaha leo. Ulifukuzwa kazini kwa hila watangazie msamaha leo. Hakikisha huna kinyongo chochote na mtu moyoni mwako. Nakuhakikishia mambo yako yataanza kwenda mbele. Unaweza ukakesha unaomba sana Mungu afungue njia ambazo umezifunga wewe mwenyewe. Leo ni siku ya wewe kuzifungua njia hizo kwa kuwatangazia msamaha waliokuumiza moyo.
Kuwa mkweli
Kuwa mkweli kwenye kila unalolifanya popote ulipo haijalishi nani anakuona nani hakuoni. Nani anakujua nani hakujui jaribu kuwa mkweli usiwe na chembe ya uongo mdomoni mwako. Watu wengi hua wanajaribu kudanganya halafu wanasingizia simu mtu yupo tayari kumdanganya mtu anaemsubiria sehemu halafu utasikia “ hizi simu hizi?” tatizo sio simu tatizo ni sisi waongo. Na hiyo ikishakua tabia yako utadanganya pia kwenye vingine. Ukiwa mkweli unakuwa huna wasi wasi kwa kila hatua unayoipiga. Ukiwa mkweli wakati mwingine huwezi kuwa na stress. Ukiwa mkweli mambo mazuri na mema yatakufuata. Nakushauri uwe mkweli kila siku UKWELI iwe ni tabia yako,.
Acha dhuluma
Usichukue mali isiyo ya halali. Mali ambayo hujaitolea jasho na wala hujapewa achana nayo. Umeokota simu nzuri sana ya mtu hakikisha unairudisha hata kama yako ni nokia tochi. Usiibe kama amri Mungu inavyotuambia kuiba nayo ni dhuluma. Umsimfanyie mwanadamu mwenzako yale usiyopenda kufanyanyiwa. Kula jasho lako ufisadi na rushwa ni wimbo wetu siku hizi sio wakubwa wala wadogo rushwa kila mahali nayo ni dhuluma hiyo maana unachukua fedha ya mtu katika njia isiyo halali. Huwezi kufanikiwa ukiwa na tabia hizi na hata ukiona umepata hizo mali kwa dhuluma hutakaa uzifurahie anza leo kuziacha. Maisha yako yakiwa yanaandamwa na lawama za watu juu ya matendo ulowafanyia huwezi kufanikiwa wala kuwa na furaha hata kama una maghorofa huwezi kua na furaha maana kuna nafsi inateseka kwa ajili ya matendo yako.
Ukiweza kuzifungua njia hizi utaendelea mbele. “Inawezekana unamwomba Mungu afungue Milango kumbe wewe ndie ulieifunga na funguo unazo umezikalia”
Jacob Mushi 2016
Tuandikie 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading