Maneno Yako Yana Nguvu ya Kuumba.

By | July 2, 2016
Maneno yale unayojinenea mara kwa mara yanakwenda kutokea kwenye maisha yako. Angalia hasa hali inayoendelea kwenye maisha yako sasa na maneno ambayo unapenda kuongea kuhusu maisha yako lazima yanaendana.

Ukiamka asubuhi na ukaanza kusema leo nimeamka vibaya siku yako itakwenda kua mbaya kweli. Ongea maneno mazuri juu ya maisha yako juu ya siku yako juu ya wiki yako na utakwenda kuona matokeo bora.

Ukiona wewe umefika mahali unasema bora mkono uende kinywani. Ujue unajitabiria hali mbaya yaani wewe pesa utakayoipata siku zote itakua ni ya kula tu.

Anza leo kuzungumza mambo makuu juu ya maisha yako jinenee baadae nzuri haijalishi hali unayopitia sasa ni ya namna gani anza kujinenea mambo makuu na yatatokea kwenye maisha yako.

 You create your world by your words. Mungu aliumba dunia kwa kusema tu na wewe unajitengenezea future yako kwa maneno unayojitamkia.

Acha kulalamika, acha kulaumu. Haijalishi wengine wanasema nini, Haijalishi wengine wanatabiri nini maisha yako ni yako. Anza kujitabiria mema leo.

Karibu sana
By: Jacob Mushi
0654726668

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *