Matokeo Ya Leo Yalisababishwa, Sababisha ya Kesho Leo.

jacobmushi
1 Min Read

Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu. Ni furaha ya kipekee sana kukuona umefika hapa tena kujifunza. Karibu sana tujifunze pamoja

Matokeo unayopata leo yanatokana na mambo uliyoyafanya siku zilizopita.

Kama una afya bora Leo ulikula vizuri na kujali afya yako kipindi cha nyuma. Hivyo ukitaka kuendelea kuwa na afya bora siku zijazo anza au endelea kutengeneza leo.

Wateja unaowapata leo ni Matokeo ya ulichokifanya siku za nyuma. Kama leo hufanyi chochote ujue kwamba huko uendako utakuja kulalamika hamna wateja.

Mahusiano mazuri unayojenga na wateja wako leo ndio yatafanya waendelee kufanya biashara na wewe.

Kitu chochote unachotaka kukitimiza maishani mwako kinaanza kufanyika leo. Haijalishi unafanya kwa kiwango gani lakini kina mchango kwenye baadae yako.

Kumbuka: Jim Rhon aliwahi kusema kwamba hatupati kile au vile tunavyovitaka tunapata vile tunavyovistahili. Haiwezekani unataka gari halafu ukaweka bidii ya kupata  pikipiki halafu ukasubiria gari. Lazima itakuja pikipiki.

Jacob Mushi,
Entrepreneur & Author,
Phone: 0654726668/0755192418
Blog:www.jacobmushi.com
Email: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading