Mti unapopukutisha majani na matunda unaweza kufikiri imepoteza kitu kikubwa sana. Mfano ndege wanapokuja na kula matunda kisha yakaanguka chini yakaoza. Wewe kwa akili zako za kibinadamu unaweza kuona ni uharibifu. Lakini kwa akili za Kimungu sio uharibifu yale matunda yaliyooza hugeuka kuwa mbolea kwa mti ule ule ulioyadondosha.

Kuna vitu ukivifanya kwenye Maisha ya watu unaweza kuona kama unapoteza lakini ni sawa na matunda haya ambayo hugeuka kuwa mbolea tena kwa mti wake. Kila unalotenda jema kwa wengine hujakukurudia katika namna ya tofauti. Hupaswi kufuatilia ujue itakuaje nitapataje, kwasababu unakuwa hujampa mtu unakuwa umemkopesha Mungu Mwenyewe.

Kama umeamua kuwatendea mema wengine usitende ili uje utendewe tena. Kama umeamua kumfanyia jambo jema fulani fanya kwa upendo na sio ili aje akukumbuke siku moja.

Ukifanya ili uje utendewe inaweza kukuumiza sana pale unapokuwa una uhitaji mkubwa halafu yeyote asikutazame. Unaweza ukapitia shida halafu wale uliowasaidia ukajaribu hata kuwakopa na wakasema hawana chochote. Lazima utajisikia vibaya na Kuumia.

Ni vyema kabisa kila jema unalotenda kwa wengine tenda kwasababu ya upendo na sio kwasababu ya kuja kutendewa tena. Usiwalazimishe watu waone wema wako. Atakaeona wema wako ni Mungu mwenyewe. Mungu akiamua kukurudishia yale uliyotenda kwa wengine hata wewe utashangaa. Kuna watu utakuwa ulishawasahau wataguswa kukusaidia bila wewe kujua.

Wema ni mbegu ambayo hatupaswi kuja kuifuata kuchungulia imefikia wapi katika ukuaji. Mbegu ambayo hatupaswi hata kidogo kuendelea kuipalilia ili tuje tuvune. Kazi yetu ni kupanda tu.

Nakutakia Kila la Kheri katika kutenda Mema.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

#usiishienjiani

www.jacobmushi.com/mentorship

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading