Kuna rafiki yangu mmoja nilikutana nae akaniambie “nyie mnaandika mbinu za mafanikio lakini hakunaga mbinu mpya zote ni zile zile tu.”  Kitu cha kushangaza ni kwamba mtu huyu bado na yeye hana chochote ambacho anakipigania yaani yupo yupo tu. Ukienda mbele Zaidi ukamuuliza kama mbinu ni zilezile wewe umeshatumia ipi ikakusaidia kati ya hizo unazozijua? Anakujibu mambo mengine ambayo hata huwezi kuaelewa.

Sasa na wewe usikubali kuwa kama huyu mtu. Kila siku kuna mambo yanagunduliwa ili kurahisisha Maisha yako. miaka michache iliyopita sikuwahi kufikiria kama ningeweza kuuza bidhaa zangu na kuwafikia wateja kwa urahisi kwa njia ya mtandao hivyo basi hizi ni mbinu mpya. Tatizo linakuja wewe unatumiaje hizo mbinu unazozijua?

Ni mbinu ipi sasa nataka uifahamu? Ili upate kile unachokitaka unapaswa kujifunza sana. Ili uweze kufika kwenye ndoto kubwa ulizonazo unapaswa kuwekeza kwenye akili yako. tafuta taarifa za kutosha na maarifa ya kutosha kwa ajili ya safari yako ya mafanikio. Hapa ndipo unaweza usinielewe unaweza kusema kusoma tu na kujifunza hakuleti mafanikio. Mimi nakwambia kufanya kazi kwa bidi pia kama hujifunzi ni sawa na unasukuma ukuta ambao unataka kuuvunja huku pembeni yako kuna nyundo ya kupasulia mawe lakini huwezi kuiona.

Unapojifunza unafungua ufahamu wako kwa upana Zaidi hivyo unajijengea nafasi ya kuona vitu ambavyo wengine hawaoni. Unapokuwa na maarifa ya kutosha unapata fursa ya kuweza kutatua changamoto unazopitia kwa urahisi Zaidi.

Popote ulipo jifunze, chochote unahcopitia jifunze, soma vitabu, nunua vitabu kila wakati. Unapokuwa na mbinu nyingi za kivita ndio unaweza kujua pa kuzitumia hasa pale adui anapokuja. Sio kila wakati utatumia bunduki kuna nyakati risasi zitakwisha utapaswa upigane ngumi kama wewe ulitumia muda wako wote kujifunza kutumia bunduki utakwama. Sio kila mahali unatumia mabomu kuna sehemu unapaswa kutumia kisu na sio ngumi. Hivyo kwa kupitia maarifa utajua ni wapi hasa pa kutumia ujuzi uliopata kwenye vitabu unavyosoma.

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading