Kama maisha yako yanategemea 90% kutoka kwenye ajira bosi wako ameyadhibiti maisha yako.
Unaweza kukuta mtu unapitia vitendo vya unyanyasaji kazini,  wakati mwingine huipendi kazi yako, inakubidi ubakie hapo hapo ulipo kwasababu hiyo kazi imekuwa kama maisha yako.
Yaani bila hiyo kazi maisha yako yanakuwa sehemu mbaya sana.

Kama maisha yako yanategemea mzazi zaidi ya 90% mzazi anakuwa na nguvu kubwa na maamuzi juu yako hata kama hata fanya chochote. Kuna wakati utakuwa unataka kufanya jambo  lakini kwasababu mzazi anahusika kwa 90% ya Maisha yako  unakua huna maamuzi ya mwisho. Wengine kwasababu mzazi ndio anakusomesha anaweza hata kukuamulia kozi gani usomee.
Ukiwa na mpenzi wako halafu unamtegemea kwenye kila kitu ikatokea amefanya usaliti unaweza shindwa kuongea kwasababu ya nguvu aliyonayo juu yako. Unakuwa na wasiwasi akiniacha au akinifukuza nitaenda wapi mimi ngoja tu nimvumilie. Labda atabadilika. Sasa wewe akijua humtegemei kwa kiasi kikubwa anakuwa na adamu kwenye matendo yake. Sisemi hivi ili wewe ukawe mbabe nyumbani ila nataka uwe na uhuru wako. Jijengee uwezo wa kujitegemea mwenyewe. Ila kiburi kisiwe juu yako. Unyenyekevu wako ubaki pale pale.
Angalau kama kuna mtu au kitu unakitegemea Kifedha kisizidi 20% au 25% ya vitu vingine. Unaweza kuwa unamtegemea mwenzako lakini basi uwe Unajishughulisha na vitu vingine vya Kukutengenezea kipato.
Angalau utegemezi usizidi 50%. Kama ni wazazi wanakusomesha chuo basi uwe na njia nyingine hata ndogo ndogo ili wasione bila wao maisha yako yatakuwa magumu.
Kama ni ajira basi uwe na njia nyingine za kukuingizia kipato.
Angalau ajira isivuke 50% ya utegemezi kwenye maisha yako.
Soma: Haya UsiYoyajua kuhusu Pesa. 

Embu tazama sasa una njia tano au nne zinazokuingizia kipato kwenye maisha yako, hata moja ikileta shida huwezi kuyumba kwa kiasi kikubwa. Wewe ndio unakuwa unadhibiti vyanzo pia unaweza kuwa na maamuzi.
Mwajiri wako akikuletea shida unaweza kuacha kazi bila ya kuwa na wasiwasi utaishi vipi. Heshima inaongezeka hata kwenye familia yako kwasababu una uwezo wa kujitegemea mwenyewe.
Usikubali Maisha yako ya kifedha yategemee kwenye kitu kimoja ambacho kikiondoka kinasababisha unayumba. Anza taratibu kujitengenezea njia mbalimbali za kipato na siku moja utafikia uhuru wa kifedha. Haijalishi upo kwenye hali ngumu kiasi gani sasa hivi suluhisho ni kutafuta njia ya kukuokoa.
KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA FEDHA NI SAWA NA KUEGEMEA MTI MKAVU KUNA WAKATI UNAWEZA KULIWA NA MCHWA.
Jipatie Blog na Utengeneze Kipato kwa Njia ya mtandao hapa
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading