KONA YA BIASHARA: Mbuyu Ulianza kama Mchicha.

jacobmushi
2 Min Read

Nionyeshe mti mmoja imara ambao umekua kwa siku chache. Ukweli ni hakuna miti mingi ambayo hukua haraka haidumu wala mashina yake sio imara kama miti inayochukua muda mwingi kukua.

Usitamani matokeo makubwa ya haraka ambayo hujayafanyia kazi utakuja kushindishwa kuyabeba au kuendeleza. Kama ambavyo tunasema mbuyu ulianza kama mchicha basi hakuna haja ya kukimbizana na wengine ambao wanakua haraka Zaidi yako.

Jipe muda wa kufikia malengo yako, jua gharama ambayo inakupasa kulipa katika muda uliojipa ili utimize hayo malengo. Biashara yeyote inayokua kidogo kidogo ina uwezekano mkubwa wa kuja kudumu kwa muda mrefu sana huku baadae.

Usishindane na mtu yeyote  hata kama ameanza juzi na wewe una muda mrefu hujui yeye anatumia nguvu gani.

Tumia nguvu kubwa mwanzoni ili baadae uje kutumia nguvu kidogo upate mavuno mengi. Usiangalie kiwango cha mavuno unayopata sasa hivi tazama kule mbele unakotaka kufika.

Wengi hushindwa kwenda mbele kwasababu ya kutamani matokeo makubwa wakati bado hawajakua. Usiwe kama watu wa aina hiyo endelea kuweka juhudi kubwa kwenye ukuzaji wa biashara  na sio kwenye matokeo. Wakati wa matokeo ukifika utafurahia matokeo makubwa.

Ili uweze kumiliki biashara kubwa inakupasa uvumilivu, kujifunza sana, bidi na kutokata tamaa. Changamoto ni nyingi lakini washindi ni wale waliozitazama ndoto zao badala ya changamoto.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading