Kokote kule utakapo kwenda utakutana na binadamu wenye tabia za tofauti na kuna kitu cha kujifunza kwao.
Wengine watakua wazuri kwako, wengine watakuumiza, wengine hawatajali chochote unachofanya au ulichonacho.
Hiyo ni kawaida ya binadamu hata wewe pia kuna unaowaumiza kwa kujua au Bila kujua. Kuna unaowafanya wafurahi kwa kujua au bila kujua.
Kuna ambao hujali wanachofanya kwa kujua au bila kujua.
Kuna ambao watakulaumu bila kujua sababu ya lililotokea au lililosababisha wewe kutokufanya kitu fulani. Wewe pia unaweza kujikuta unawalaumu wengine wamefanya kitu fulani vibaya bila kujua sababu kwa undani ya chanzo cha tatizo lenyewe.
Hao ndio binadamu jifunze kila unapokwenda na kwa kila unaekutana nae.
Jacob Mushi
Inuka Uangaze