Habari ndugu msomaji wa mtandao huu karibu tena katika makala ya leo. Ni matumaini yangu unaendelea vyema na maisha yako. Leo ningependa tujiulize swal moja… Msaada wako utatoka wapi wakati wa shida? Karibu sana.

Katika hali ya kawaida najua hii wengi wanayo unapopata tatizo la kifedha leo ni nani wa kwanza kumfikiria wa kukupatia fedha hizo? Sio vibaya kuwa na hali hii ni kutokana na mazoea tuliyojijengea katika maisha ndio maana kuna wakati ukipata tatizo mtu anaweza kukufata akakwambia si umfate fulani akusaidi? Ukweli ni kwamba yule unaedhani ndio msaada wako na yeye ana mambo yake ya kufanya. Jiulize yeye anategemea wapi msaada?

Kitu cha muhimu cha kufanya ni kumtegemea Mungu peke yake na pia tumia akili na nguvu alizokupa. Si kwambii ukipata tatizo usiombe msaada bali ingefaa kabla ya kuomba msaada uwe umeshaanza kutatua tatizo hilo. Huo ndio ukweli tujitahidi kabla ya kuomba msaada wowote chukulia kua umwombaye nae ana matatizo makubwa zaidi ya yako.

Tulizaliwa tukafundishwa kuomba  sasa tuna serikali ambayo inaomba misaada nje lakini hiyo yote ilianzia kwenye ngazi ya familia. Sasa hivi tuna kizazi kinachokua tutakua kwenye hali mbaya zaidi. Muhusika wa kwanza na mtatuzi wa matatizo yako ni wewe mwenyewe. Wahusika wakuu wa kuboresha maendeleo ya nchi hii ni sisi Watanzania wenyewe. Tena maandiko yanasema heri kutoa kuliko kupokea. Kabla hujaomba angalia kwanza wewe umeombwa na wangapi kama hakuna basi acha kwanza.

Tumaini la pekee ni Mungu tu yeye ndie msaada wa pekee kwa mwanadamu hakuna mwingine kama yeye. Tukimtegemea Mungu hatuwezi kujuta kamwe. Maana yeye  anasema ni msaada tele wakati wa mateso. Tunamuhitaji yeye kila siku kwenye maisha yetu.

“Ukitaka kuishi bila kuvunjwa moyo usitarajie/usitegemee chochote kutoka kwa mtu isipokua wewe peke yako ” Tegemea kwa Mungu  kwani yeye sio mwanadamu
“Mungu kwetu ni kimbilio na nguvu msaada tele utakaonekana wakati wa mateso” Zaburi 46:1-3, zaburi 37:25
Mtegemee Mungu Peke yake.

Asante sana kwa kujifunza pamoja na mimi karibu sana.
Tuma maoni yako au ushauri kwa no. 0654726668
E-mail riseshine500@gmail.com
Tembelea ukurasa wetu facebook Rise and Shine Tz

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading