Kuna wimbo ambao umekuwa unaimbwa na watu wengi sana hasa linapokuja swali ni kwanini hujaweza kuanza biashara au kile ambacho unataka kufanya.
Wimbo huu umekuwa ndio kikwazo kikubwa cha wengi kiasi kwamba wanabaki pale pale walipo siku zote.
Sina Mtaji ni neon ambalo kama kweli una nia na mafanikio basi hutakiwi kulitamka mdomoni mwako tena kuanzia sasa. Tumeshasema  mara kadhaa kwamba mtaji sio pesa pekee bali ni mkusanyiko wa vitu vyenye thamani ambavyo vinakuwezesha wewe uanze biashara au kile unachokitaka.
Sasa kama unasema huna mtaji maana ni kwamba umesema huna chochote kabisa. Yaani hata wewe mwenyewe ni sifuri. Kwasababu mtaji unakujumuisha na wewe pia, kuanzia maarifa uliyonayo, uwezo ulionao, nguvu ulizonazo na watu unaowafahamu. Sasa kusema huna mtaji ni kwamba umejidhalilisha mwenyewe.
Badilisha msamiati wa sina mtaji uanze kusema umepungukiwa vitu Fulani tu. Hii itaonyesha kwamba unajua unachotaka kwenda kukifanya.
Mtu anaesema hana mtaji maanake ni kwamba hata hajui kile anachokwenda kukifanya. Ukiweza kuchanganua vizuri kile unachotaka kwenda kufanya utagundua una vitu vingi tayari ila umepungukiwa vitu vichache tu.
Ndugu yangu badilika la sivyo kusema huna mtaji, au huna sijui nini hakukubadilishii chochote kwenye Maisha yako.
Anza sasa kujitengenezea msamiati mpya wa Maisha yako. Kama umepungukiwa vitu basi kuna namna ya kuvipata hivyo.
Mwaka 2018 unatakiwa uanze kile ambacho umekuwa unasema siku nyingi sana kwamba utakianza.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading