Yapo mambo ambayo ni msingi wa Maisha bora ya kila mwanadamu, kama ukiweza kuyafanyia kazi vizuri utaishi kwa furaha na amani hapa duniani siku zote. Ni kweli yapo mambo mengi mabaya yanatokea bila sisi kujua na tunakuwa hatuna uwezo wa kuzuia lakini ukiweza kufuata hii misingi utaweza kuwa na Maisha bora.

Mambo haya ndio yanayofanya Maisha ya mwanadamu kuwa na ukamilifu, bila hayo utakuta mtu anafanya mabaya, na kuwaumiza wengine. Naomba haya uyaweke katika vipaumbele vyako vya Maisha na uweze kuvifanyia kazi.

Mungu.

Kama umekuwa unafuatilia haya mafundisho utakuwa umeona kwamba siachi kumzungumzia Mungu, naamini na wewe pia unaamini kuhusu Mungu kwa Imani yeyote uliyonayo. Ni lazima uwe na mahusiano bora na Mungu wako. Njia ya kuweza kuwa na mahusiano hayo bora ni wewe kuishi kusudi la kuwepo hapa duniani. Yeye amekuleta hapa duniani amekupa vipawa vya aina mbalimbali ili uweze kumbariki ni pale tu utakapoanza kuishi vile anavyotaka.

Afya.

Afya yako ndio chanzo cha nguvu ambazo unaweza kuzitumia kuishi na kufanya chochote hapa duniani. Unapaswa kuwa na afya bora katika Roho yako. Ili uwe na afya bora ya roho unapaswa kusali na kumuomba Mungu kila wakati. Hii itakusaidia uwe mtu mwema na utaepushwa na mabaya katika mafanikio yako.

Pia unapaswa kuwa na afya bora ya Akili yako, soma vitabu juu ya Mungu (Biblia na Vingine), Afya, Mahusiano, Fedha, Biashara. Hakikisha unapata ufahamu sana kwenye kile ambacho umechagua kukifanyia kazi yaani lile kusudi la Mungu Kukuleta hapa duniani.

Tatua unapaswa kuwa na Afya ya Mwili, lazima uwe na afya bora ili uweze kufanya kazi kwa bidii, kufurahia mahusiano na pia kuishi vizuri hapa duniani. Fanya mazoezi, kula vizuri, pumzika vizuri.

Mahusiano.

Bila mahusiano unakuwa kama umepoteza matumaini, kuna watu unaowapenda kama ndugu zako, mume, mke, Watoto na marafiki. Hawa ni watu wa muhimu sana ambao wanakuwa na wewe mara kwa mara. Ukikosa mahusiano bora na hawa utaona dunia ni mbaya na utakosa hata matumaini ya kuishi.

Uhuru wa Kifedha.

Ni lazima uwe na uhuru wa kifedha ili uweze kuishi yale Maisha ambayo unayataka. Maisha yasiyo na vikwazo, Maisha yasiyo na hofu ya kesho itakuaje sina pesa. Katika Maisha yako pambana hakikisha una uwezo wa kifedha. Hakikisha una vyanzo visivyopungua vitatu vya kukuingizia kipato. Inaweza kuwa kile ambacho Mungu ameweka ndani yako, Inawezekana ukawa na biashara na pia ukawekeza katika sehemu nyingine.

Hakuna mtu mwenye amani halafu ana madeni hadi kwa majirani zake. Hakuna mtu mwenye amani ambaye ana wasiwasi wa kesho atakula nini. Huwezi kuwa na amani kama unawaza sana juu ya ada za Watoto. Hivyo basi endelea kupambana uweze kufikia uhuru wa kifedha.

Haya ndio mambo manne ambayo ukiweza kuyawekea vipaumbele kwenye Maisha yako basi utaishi Maisha bora sana.

Jinuge na Program ya Mwaka wa Mafanikio Bonyeza Linki mwishoni mwa Makala hii.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading