Mambo maovu yote yanayoendelea duniani yanasababishwa na watu wengi kuishi bila kutambua makusudi ya wao kuwepo duniani. Mtu anapozaliwa anakua na uwezo mkubwa sana ndani yake kwa ajili ya kumwezesha kulitimiza kusudi lake na anaposhindwa kuzitumia nguvu hizo Shetani huzitumia. Ndio maana tunaona watu wanakua waovu na wakitenda mambo mabaya yasiyofaa hiyo yote ni nguvu zilizokosa matumizi yake halisi. Hakuna mwanadamu alieumbwa ilia je kua jambazi au kahaba, hakuna alieumbwa ili awe muuaji, mlevi, mbakaji, mzinzi, na mengine yote maovu unayoyafahamu. Vyote hivi vinatokea kwasababu ya watu kutokutambua makusudi yao ya kuwepo duniani.
Neno la pekee nililonalo kwa ajili yako ni kwamba hujachelewa bado una nafasi ya kuanza kuishi kusudi lako haijalishi una umri gani sasa wako waliogundua makusudi yao wakiwa wazee kabisa. Haijalishi umeshakosea kiasi gani umetenda uovu kiasi uhai ulionao ndio kitu cha kwanza kutumia. Kuwepo kwako hai ni sababu tosha kwamba bado unayo nafasi ya kuishi na kulitimiza kusudi lako. Anza leo maana ndio pekee uliyonayo.
Kingdom of Success
Jacob Mushi
jacob@jacobmushi.com