Kila mwanadamu ana maamuzi ya mwisho juu chochote anachokiwaza na maamuzi anayoyachukua. Yaani kama umeamua kuamka saa kumi na moja ni wewe mwenyewe unaamua kutokuamka au la hakuna mtu mwingine anaweza kuja kukufanya uamue kuendelea kulala au kuamka ni wewe unakua na maamuzi yote hata kama mtu atakuja kukuamsha kwa nguvu bado una maamuzi ya kuendelea kulala au kuamka.

Tukiachana na kuamka tukija kwenye mambo ambayo yanaleta mabadiliko kwenye maisha yetu, mfano kama umepata wazo bora la biashara au umekutana na jambo likakuhamasisha sana, wewe pekee ndie unakua na maamuzi ya kuahirisha au kuchukua hatua hakuna mtu mwingine ataweza kuja kukufanyia maamuzi hata akija mtu anaehamasisha kiasi gani akazungumza na wewe maamuzi bado yanakua juu yakow ewe peke ndie mwenye uwezo wa kukataa au kukubali.

Lengo la mimi kuandika juu ya uwezo wa maamuzi na nguvu iliyoko nyuma yake ni kukuonyesha kwamba wewe ndiye mwenye kila sababu na uwezo wa kubadilisha maisha yako mwenyewe kuna wakati tunahitaji kusukumwa na kuhimizwa, kusoma Makala kama hizi za kuhamasiha, kusikiliza audio za kuhamasisha, kuhudhuria semina mbalimbali, vyote hivyo tunafanya kujenga ufahamu mzuri lakini sio kwenye kuchukua hatua kuchukua hatua ni wewe unaaamua. Maamuzi juu ya chochote unachokiingiza kichwani kwako ni wewe unayafanya sio kile kilichoingia kinaamua.

Unaweza kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi itakuletea matokeo bora,

Ukifanya maamuzi sahihi wakati usio sahihi unaweza kusababisha majanga makubwa pia kama hasara.

Ukifanya maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati sahihi bado hutapata matokeo unayoyataka.

Ukifanya maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati usio sahihi ni kujiongezea matatizo juu ya maisha yako.

  Ongeza uwezo wako wa kulielewa jambo unalotaka kufanyia maamuzi hii itakuasaidia sana unapotaka kufanya kitu chochote fikiri kwa makini fanya maamuzi kwa makini maana maamuzi unayoyachukua leo ndio yanaweza kua sababu ya wewe kutoka ulipo kwenda sehemu bora Zaidi maishani mwako.

Nguvu Uliyonayo ni kubwa sana itumie vyema ili upate matokeo bora.

Asante sana.
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading